Maelezo kuhusu virusi vya korona

Ukurasa huu ulisasishwa mwisho 5/25/2020. Kwa sasisho baada ya hiyo tarehe, tafadhali nenda kwa ukurasa wa Kiingereza

Msaada kwa wahamiaji, wakimbizi na watafutao hifadhi ili waelewe virusi na namna ya kukaa salama.

Kuna virusi vipya vinavyoenea duniani kote ambavyo vinasababisha ugonjwa wa COVID-19. Watu kila mahali wanafanya kazi kwa umoja ili kujaribu kupunguza kasi ya kusambaa kwa virusi hivi na kuokoa maisha. Kurasa hizi zinaelezea taarifa za afya zilizotafsiriwa kutoka vyanzo vinavyoaminika. Utapata pia taarifa muhimu mpya kuhusu kanuni za uhamiaji, fedha, na msaada kwa wazazi. Tuko hapa kusaidia. Ukihitaji taarifa zaidi, unaweza kuuliza [email protected].

hand washing illustration

Kaa kwa afya njema

Jifunze namna unavyoweza kutunza afya yako na ya familia yako. Jilinde mwenyewe na wenzio dhidi ya maambukizi. Elewa miongozo na kile cha kufanya. Jifunzi namna ya kutunza afya yako.

illustration of someone sick in bed

Pata usaidizi kama wewe ni mgonjwa

Sote tunahofia nini kitatokea tukiambukizwa. Lakini kila mmoja anaweza kupata msaada. Jiandae mwenyewe na familia yako. Tafuta cha kufanya mtu akiambukizwa. Pata msaada

clipboard illustration

Kwa wahamiaji, wakimbizi na watafutao hifadhi

Kila mmoja hivi sasa anahofia. Lakini ukiwa mhamiaji, mkimbizi, au mtafuta hifadhi Marekani, unaweza kuwa na hofu za ziada. Ukurasa huu una taarifa ambazo ni muhimu kwa jamii za wahamiaji. Pata taarifa kwa waliowasili hivi karibuni

illustration of parents and children

Kwa wazazi na watoto

Huu ni muda mgumu sana kwa wazazi. Lakini kuna njia za kupata msaada kwa wazazi na kusaidia watoto wakae kwa afya na wahisi salama. Pata taarifa za wazazi na watoto

Money illustration

Pata msaada ukipoteza kazi yako

Umepoteza kazi yako? Tafuta ikiwa unaweza kupata msaada wa serikali na cha kufanya ikiwa hustahili. Pata msaada

newspaper illustration

Kaa salama kwa kupata taarifa za kweli

Kuna taarifa nyingi kuhusu virusi vya korona. Utajuaje ipi ni ya kweli na ipi si ya kweli? Tunaweza kukusaidia kukaa salama mbali na taarifa za uongo na utapeli. Pata taarifa sahihi

Taarifa hizi zinatoka kwa vyanzo vya kuaminika, kama vile Kituo cha Kudhibiti Magonjwa na Shirika la Afya Duniani. USAHello haitoi ushauri wa kisheria au kitabibu, wala rasilmali zetu zozote zisichukuliwe kuwa ni ushauri wa kisheria au kitabibu. Taarifa zetu za afya zimekaguliwa na mjumbe wa bodi ya USAHello Tej Mishra, mtaalamu wa afya ya jamii na epidemiolojia ya Marekani.

FindHello CTA map
FindHello

Tumia FindHello kutafuta msaada na rasilmali karibu nawe. Tafuta ushauri wa ajira, wanasheria, tiba, madarasa ya Kiingereza na huduma nyingine katika jamii uliyoko.

Anza kutafuta