Ukurasa huu ulisasishwa mwisho 5/25/2020. Kwa sasisho baada ya hiyo tarehe, tafadhali nenda kwa ukurasa wa Kiingereza
- English (English),
- አማርኛ (Amharic),
- العربية (Arabic),
- မြန်မာစာ (Burmese),
- 简体中文 (Chinese),
- 繁體中文 (Chinese (Traditional)),
- فارسی (Persian),
- Français (French),
- Italiano (Italian),
- 日本語 (Japanese),
- Ikinyarwanda (Kinyarwanda),
- 한국어 (Korean),
- Português (Portuguese, Brazil),
- Русский (Russian),
- Somali (Somali),
- Español (Spanish),
- Tagalog (Tagalog),
- ไทย (Thai),
- Türkçe (Turkish),
- Українська (Ukrainian),
- اردو (Urdu),
- Tiếng Việt (Vietnamese)
Sote tuna wasiwasi kuhusu virusi vya corona. Ikiwa wewe ni mhamiaji, mkimbizi au muomba hifadhi katika nchi ya Marekani, unaweza ukawa na wasiwasi zaidi. Ukurasa huu unaelezea baadhi ya mada muhimu katika jamii ya wahamiaji. Unaweza pia kupata maelezo zaidi kuhusu ICE, USCIS, na mabadiliko mengine katika taratibu za uhamiaji kwa sababu ya COVID-19.
Ni nini hasa kinachokupa wasiwasi?
Wageni wengi wanakuja Marekani kutokana na hali mbaya nchini mwao. Ni vigumu sana kuiamini serikali. Pia, kuna sintofahamu kutoka uongozi wetu wa Marekani katika wakati huu mgumu. Je, inatupasa kuchukua hatua zipi na kumuamini nani?
Tunaweza kuamini habari afya kutoka serikalini
Kituo cha Kuthibiti Magonjwa (CDC) ni wakala wa serikali ya kimarekani inayoongozwa na wanasayansi wa kitaalamu. Wanahatarisha maisha yao katika kutafuta uelewa wa magonjwa kama COVID-19 ili kuikinga umma nzima. Ni muhimu tukiamini taarifa zao katika nyakati hizi.
Unaweza ukaamini mamlaka na huduma za afya katika jamii zenu
Kila mkoa, jimbo na mamlaka ya jiji zina wakala wa afya ya jamii. Mamlaka ya afya katika mkoa wako haijali masuala yako ya uhamiaji. Wanajali afya yako. Unaweza kuwaomba wakusaidie.
Marekani, sheria inasema kwamba hamna chumba chochote cha matibabu ya dharura hospitalini kitakacho kukufukuza kwa sababu ya ukosefu wa vibali halali au kwa sababu huwezi kulipia matibabu. Ukiwa mgonjwa, tafuta msaada. Lakini kwa sababu COVID-19 inambukiza sana, piga simu 911, katika hospitali au zahanati iliyokaribu kwanza.
Una haki ya kupata matibabu nchini Marekani bila kujali uhalali wako. Pia una haki ya kuwa na bima ya afya. Soma kuhusu haki yako ya kupata matibabu katika lugh ya: Kiingereza, Kiarabu, Kiamharic, Kiburmese, Kichina, na Tagalog..
- Tafuta kliniki inayotoa huduma za bure (huduma za kiafya kwa watu ambao hawawezi kujilipia).
- Tafuta zahanati (huduma za matibabu ambazo zinatoza viwango ambavyo ni nafuu kwako). Vituo vingi vya afya vinatoa huduma za bure za kupima COVID-19 kwa watu wote.
- Mkoa wa California una bima ya afya inayoitwa Medi-Cal kwa ajili ya wahamiaji walio na umri chini ya miaka 25 ambao hawana vibali halali.
Marekani, watu wanalengwa kwa sababu ya hofu ya COVID-19. Unaweza kufanya nini?
- Unaweza ukatoa taarifa kuhusu ubaguzi katika manispaa yako au kwa wakala wenye uhusiano na ACLU.
- Unaweza kuwakilisha ripoti ya tukio katika halmashauri ya Sera na Mipango cha Asia Pacific.
- Ukibaguliwa kazini, unaweza kuwasilisha malalamishi kupitia serikali ya Marekani.
- Pata habari kuhusu unyanyapaa kutoka Kituo cha Kuthibiti Magonjwa.
- Pata rasilimali dhidi ya unyanyapaa kutoka mkoa wa Washington.
- Jifunze cha kufanya mtu akikitisha.
- Unaweza pia kujifunza kuhusu haki zako.
USAHello haitaweza kutoa ushauri wa kisheria au wa uhamiaji. Lakini tunaweza tukakuunganisha na wataalamu wa kutoka ushauri wa uhamiaji na kisheria ambao wanaweza kukusaidia:
ImmigrationLawHelp.org
ImmigrationLawHelp.org inasaidia wahamiaji wenye mapato ya chini na kupata msaadwa wa kisheria. Unaweza kutafuta ushauri wa kisheria katika tovuti yao kwa kutumia nambari yako ya posta . Unaweza pia kutafuta kupitia kituo cha mahabusu kama wewe au ndugu yako amewekwa kizuizini nchini Marekani.
Boundless
Ofisi nyingi za kiserikali zinazoshughulikia mambo ya uhamiaji na vibali zimefungwa. Boundless ni tovuti inayoaminika kwa kutoa maelekezo ya maombi ya uraia na kadi za kijani. Soma maelezo yake kuhusu jini gani virusi vya corona vinavyoathiri mahojiano, hati, na maombi ya masuala mbalimbali.
United WeDream
Shirika la United WeDream linasaidia wamarekani wasio na vibali. Wanatoa habari kuhusu kufungwa kwa ofisi za uhamiaji (USCIS) na maombi mapya kupitia tovuti ya DACA (shirika linalotoa misaada na vibali vya kazi kwa wahamiaji vijana) .
Kituo cha USCIS kinasema kwamba upimaji, ukingaji, au matibabu ya COVID-19 hayatatumika kwa mashtaka ya umma. Ukiwa mgonjwa, usiwe na hofu ya kutafuta msaada kwa sababu ya gharama za malipo kwa umma .
Ukipoteza kazi yako kwa sababu ya dharura, au shule yako ikifungwa, unaweza kuandika maelezo ya kuambatana na maombi yako ya hati na vibali. Halafu, ikikubidi kukubali msaada wa kutoka serikalini, inapaswa usihesabike kama shtaka la umma.
Unaweza kusoma zaidi kuhusu mashtaka ya umma katika tovuti ya USAHello .
Sheria zote zilizo muhimu ni sawa katika sehemu zote za Marekani:
- Epuka mahusiano yeyote na watu ambao hawaishi nawe.
- Kaa nyumbani kadri itakavyowezekana na pia watoto wako wakae nyumbani.
- Unaweza ukatoka nje kufanya mazoezi au kwenda kununua chakula na dawa lakini inabidi ukae umbali wa futi sita kutoka kwa watu wengine.
- Funika pua na mdomo wako ikikubidi kuwa karibu ya zaidi ya futi 6 na watu ambao huishi nao.
- Usiende kazini au usitoke nyumbani ukiwa mgonjwa.
- Dumisha usafi. Usafi bora unamaanisha kunawa mikono yako, kutumia tishu kukohoa na kupiga chafya, kutokugusa uso wako na kusafisha maeneo yote.
Kila mkoa una sheria zake. Lakini ukifuata maelekezo muhimu yaliyo hapo juu, utajikinga na kuwakinga wengine katika mahali unapoishi. Pata habari zaidi kuhusu jinsi ya kuishi kwa afya.
Mwongozo huu, ulioundwa na HIAS, unatoa habari kwa wakimbizi, watafutaji wa hifadhi, asylees na wahamiaji wengine kuhusu haki zako wakati wa muda huu wa uhakika.
- Jua haki zako katika Kiarabu
- Jua haki zako kwa Kiingereza
- Kujua haki zako katika Farsi
- Kujua haki zako katika Kifaransa
- Kujua haki yako katika Urusi
- Jua haki zako katika Kihispania
- Jua haki zako kwa Kiswahili

Sasisho na mabadiliko kwa sababu ya COVID-19
Kumekuwa na mabadiliko na ufungaji wa vituo vingi vinavyohusiana na uhamiaji kwa sababu ya mlipuko wa COVID-19. Haya ni sasisho kuhusu wahamiaji, wakimbizi na waomba hifadhi:
- Utawala wa Marekani imetoa amri kuu ya kuacha Visa vipya vya uhamiaji (kadi za kijani) kutoka Aprili 23, 2020, kwa siku 60. Utaratibu unatumika kwa watu wa nje ya Marekani. Wafanyakazi wa afya, wafanyakazi wa kilimo na baadhi ya wafanyakazi wengine bado watakubaliwa kupata viza. Wanandoa na watoto chini ya umri wa miaka 21 ya wananchi wa Marekani bado kuruhusiwa kupata viza. Watu ambao tayari wana viza ya wahamiaji au nyaraka halali za kusafiri bado wanaweza kuja. SIVs na wanachama wa majeshi ya Marekani bado wanaweza kuja.
- Mnamo Machi 2020, USCIS ilifuta miadi na ofisi zilizofungwa isipokuwa kwa dharura. USCIS inafungua ofisi zingine mnamo Juni 4. Vituo vya Msaada wa Maombi bado havipo wazi.
- Ikiwa mahojiano yako ya kimbari yamefutwa, utapata notisi na tarehe mpya ya kuteuliwa.
- Ikiwa sherehe yako ya uraia ilifutwa, utapata notisi ya kuweka tarehe mpya ya sherehe.
- Ikiwa una mahojiano mengine ambayo yalifutwa, unapaswa kupokea notisi mpya ya uteuzi kutoka kwa ofisi ya shamba lako.
- Ikiwa unayo Menejimenti au miadi mingine, unahitaji kupanga ratiba mwenyewe wakati ofisi ya shamba imefunguliwa. Utahitaji kutumia kituo cha mawasiliano cha USCIS.
- USCIS ina sheria mpya katika ofisi zote kuzuia kuenea kwa COVID-19. Lazima kuvaa mask na kufuata maelekezo juu ya utaftaji wa kijamii.
- Tafadhali soma ukurasa wa coronavirus wa USCIS kwa habari zaidi. kuhusu kufunguliwa kwa ofisi, mahojiano na miadi.
- USCIS inasema kwamba huduma matibabu ya COVID-19 sio shtaka la umma.
- USCIS ilitangaza kwamba itatumia tena takwimu ilizo nazo kushughulikia Kurefusha Idhini ya Stakabadhi ya Ajira (EAD). Soma maelezo.
- Ofisi ya Utendaji ya Idara ya Sheria ya Marekebisho ya Uhamiaji (EOIR) imefunga korti nyingi za uhamiaji isipokuwa kwa usikilizaji wa wafungwa. Fahamu mabadiliko ya EOIR.
- Kituo cha Visa cha Taifa (NVC) kitajibu tu mahitaji ya dharura. Kama unahitaji isiyo ya dharura, tumia kifaa cha CEAC, lakini unaweza kuwa na ugumu wa kupata jibu.
- ICE inaendelea kukamata watu, lakini ICE imesema haitakamata watu kwenye vituo vya afya na hospitalini. Pia wamepeleka mbele muda wa baadhi ya watu kujiwasilisha wenyewe. Soma kile ambacho ICE inasema kuhusu utekelezaji kwenyeukurasa wa ICE wa taarifa kuhusu virusi vya corona.
- ICE imechapisha taarifa kwa watu kuhusu Mpango wa Wanafunzi na Wageni wa Mabadilishano (SEVP) kuhusu athari ya virusi vya corona kuhusu shule na wanafunzi.
- Wanaotafuta hifadhi wafikapo kwenye boda wana rudishwa. Wanarudishwa Mexico au nchi zao. Hii inajumuisja watoto wasiosindikizwa. Soma sasisho za wanaotafuta hifadhi.
- Idara ya Taifa ya Marekani ilisema kwamba Marekani itasimamisha kupokea wakimbizi.
- Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM) na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) walisema kwamba wakimbizi watatumwa kwenda nchi zingine. Matangazo yalisema kwamba safari itaanza tena mapema iwezekanavyo.
Taarifa hiyo inatoka kwenye duru, kama vile USCIS, na Idara ya Usalama wa Nyumbani, HIAS, na CLINIC. USAHello halitoi ushauri wa kisheria au kimatibabu, wala rasilimali zetu hazikusudiwi kuchukuliwa kama ushauri wa kisheria au kimatibabu.