Ukurasa huu ulisasishwa mwisho 5/25/2020. Kwa sasisho baada ya hiyo tarehe, tafadhali nenda kwa ukurasa wa Kiingereza
- English (English),
- አማርኛ (Amharic),
- العربية (Arabic),
- မြန်မာစာ (Burmese),
- 简体中文 (Chinese),
- 繁體中文 (Chinese (Traditional)),
- فارسی (Farsi),
- Français (French),
- Italiano (Italian),
- 日本語 (Japanese),
- Ikinyarwanda (Kinyarwanda),
- 한국어 (Korean),
- Português (Portuguese, Brazil),
- Русский (Russian),
- Somali (Somali),
- Español (Spanish),
- Tagalog (Tagalog),
- ไทย (Thai),
- Türkçe (Turkish),
- Українська (Ukrainian),
- اردو (Urdu),
- Tiếng Việt (Vietnamese)
Huu ni wakati mgumu sana kwa wazazi. Lakini kuna njia za kupata usaidizi kwa wazazi na watoto kubaki kwa afya na kujisikia salama.
Kwa wazazi
Shule zinaweza kukusaidia
Ingawa watoto wanaweza kutougua sana, wangali wanaweza kupata virusi. Shule za Marekani zimefungwa kusimamisha maenezi ya virusi. Huenda ulipata notisi kutoka kwa shule ya mtoto wako kuhusu kufungwa huko. Huenda ilikuwa kwa njia ya simu, baruapepe au tovuti ya shule.
Je, una hitaji la kuzungumza na mtu katika shule ya mtoto wako? Huenda usijue mtu wa kumpigia. Ili kupata shule ya mtoto wako, andika “pata shule yangu ya karibu” kwenye brausa yako na uchague kutoka kwenye orodha inayokuja. Ikiwa habari unayohitaji haipo kwenye wavuti ya shule, piga simu nambari iliyo kwenye wavuti.
Wafanyakazi wa shule bado wanafanyakazi. Waalimu wanatoa”masomo ya umbali.” Hii inamaanisha wanaendelea kufundisha wanafunzi ingawa wako nyumbani. Unaweza wasiliana na shule ya mtoto wako ukiwa na maswali kuhusu masomo ya umbali.
Shule nyingi zimetia somo yao mtandaoni kwa wanafunzi wao kusomea nyumani. Wengi pia wana mfumo kwa familia ambao hawana mtandao na tarakilishi. Ikiwa wana mfumo, unaweza kuchukua vifaa kutoka shuleni kwa mtoto wako kusoma nyumbani. Wafanyakazi wa shule wanaweza kukuambia jinsi ya kufanya hivyo. Ikiwa unatumia baruapepe, labda unayo anwani ya baruapepe kwa mwalimu wa mtoto wako. Ikiwa huna, wasiliana na shule kwa simu.
Ikiwa watoto wako walipokea chakula shuleni ilipokuwa imefunguliwa, bado wanaweza kupata chakula kutoka kwa shule. Shule yako au wilaya ya shule itakupa habari. Ikiwa hujapata habari, wasiliana na shule.
Shule hizo zitabaki zimefungwa hadi iwe salama kwao kufunguliwa. Uamuzi wa kufungua shule utafanywa na maafisa wa afya ya umma. Pata idara yako ya afya. Ukurasa huu umesasisha habari kuhusu wakati shule zitafungua katika kila jimbo.
Baadhi ya vituo vya mchana na shule zinabaki wazi kwa wafanyakazi wa dharura na muhimu. Ukiwa mfanyakazi muhimu, unaweza kupata taarifa kutoka idara yako ya afya au shule.
Ushauri kwa wazazi walio na watoto nyumbani
CDC ina ushauri huu kwa wazazi:
- Kuwa mtulivu na mhakikishi.
- Kuwa tayari kusikiliza na kuzungumza.
- Epuka lugha inayoweza kulaumu wengine na kusababisha unyanyapaa.
- Kuwa makini na kile watoto wanaona au kusikia kwenye runinga, redio au mtandaoni.
- Wape watoto taarifa ambayo iko aminifu na kamilifu.
- Wafunze watoto jinsi ya kuwa na afya.
Save the Children linahudumia watoto kote duniani. Wataalam wake wa watoto wana vidokezo ambavyo unaweza kutegemea juu ya jinsi ya kuzungujza na watoto wako kuhusu virusi vya corona na COVD-19:
- Uwe na taarifa na ushiriki ukweli.
- Jenga mbinu yako kulingana na mtoto wako – fikiria ikiwa habari zaidi huwafanya kuwa na wasiwasi zaidi au la.
- Shughulikia mada hiyo kwa urahisi na kwa utulivu – watoto wanapata habari zao kutoka kwako.
- Muulize mtoto wako kile anachokijua, jibu maswali yake na ushughulikie habari potofu.
- Thibitisha hisia zao, huku ukiwahakikishia – “Ninaelewa hii inaweza kuwa ya kutisha. Tunachukua hatua za kuwa na afya njema, na tumejiandaa vyema. ”
- Wakumbushe kile kilicho kwenye uwezo wao – kunawa mikono vizuri kila mara, kukohoa na kupiga chafya kwenye kiwiko chao, kupata usingizi mwingi, nk.
- Mithilisha usafi bora, na jaribu uwe wa kufurahisha! Imba wimbo unaopenda huku ukisugua mikono kwa sabuni na maji kwa angalau sekunde 20.
- UNICEF inazo taarifa kwa wazazi katika Kiarabu, Kichina, Kiingereza, Kifaransa, na Kihispania.
- Hapo kuna mbino kadhaa kwa wazazi kutoka Shirika la Afya Duniani katika Kiingereza na katika Kihispania. Tutaongeza lugha zaidi zinapopatikana.
- Khan Academy inatoa mafunzo ya bure mtandaoni kwa umri wote. Kurasa zake kwa wazazi zipo katika lugha nyingi.
- Chuo cha Child Mind Institute kina mbinu kwa wazazi na fursa kwa wazazi ya kusimulia kwa video chat na wataalamu.
Kwa watoto
Hapa kuna mambo kadhaa unaweza kuonyesha wanao kwa kompyuta au simu ya mkono.
- Soma kitabu maalumu COVI book katika lugha 25. Kitasaidia kila mtu ndani ya jamii kujisikia vizuri zaidi! Unaweza kupakua pdf au kusomea kwenye mtandao.
- Tazama video toka Sesame Street kuhusu usafi juu ya virusi vya korona.
- Soma kitabu cha picha kuhusu virusi vya korona katika Kiarabu.
- Soma “The Flying Scientist” (tafsiri: “Mwanasayansi anayeruka”) katika Kiarabu au katika Kingereza.
- Pata taarifa kuhusu virusi vya korona kwa watoto katika Kihispania.
- Tafuta habari za Sawanya kwa watoto wa umri wa miaka 3 – 6 na 7 – 12 na kwa vijana katika lugha 35.
- Colorín Colorado anazo rasimimali za kielimu katika Kingereza na katika Kihispania.
- Booksmart ni programu iliyo na mamia ya vitabu katika Kingereza, Kiarabu, Kihindi na Kihispania.
- Khan Academy ina darasa za bure kwenye mtandao kwa watoto wa umri wa toka myaka 4 hadi 18. Una weza kugeuza lugha kwa upande wa chini wa ukurasa. Kwa kuanza, nenda kwa ukurasa kuhusu masomo ya mbali wakati wa mafungo ya shule.
- Learning Heroes ina rasilimali kwa watoto na kwa wazazi kwa Kiingereza na Kihispania.
- Pakua orodha ya tovuti nzuri na programu kwa watoto wadogo.
- Lingokids ni programu ya kujifunza lugha ambayo inaruhusu watoto kucheza michezo ya kujifunza Kiingereza. Unaweza kuitumia kwenye simu za mkononi na kompyuta kibao. Pamoja na USAHello, watoto wako wanaweza kutumia LingoKids kwa bure.
Taarifa hutoka kwenye mahali pa kuaminika, kama UNICEF, Save the Children, the Kituo cha Kudhibiti Magonjwa na Shirika la Afya Duniani. USAHello halitoi ushauri wa kisheria au kimatibabu, wala rasilimali zetu hazikusudiwi kuchukuliwa kama ushauri wa kisheria au kimatibabu.