Pata usaidizi ukiwa mgonjwa

Ukurasa huu ulisasishwa mwisho 5/25/2020. Kwa sasisho baada ya hiyo tarehe, tafadhali nenda kwa ukurasa wa Kiingereza

Sote tunaogopa nini kitatokea ikiwa tutakuwa wagonjwa. Lakini unaweza kupata usaidizi ukiwa mgonjwa. Jitayarishe mwenyewe na familia yako ikiwa mtu atakuwa mgonjwa.

Dalili ni zipi?

Dalili ni ishara kuwa wewe ni mgonjwa. Sio kila mtu ambaye ana COVID-19 anapata dalili zote. Watu wengi huwa wagonjwa halafu wanapata nafuu bila kuhitaji huduma ya matibabu. Watu wachache hawana dalili. Watu wengine wanapata dalili kali sana.

Dalili kuu za COVID-19 ni:

  • Joto jingi
  • Kikohozi
  • Matatizo ya kupumua
coronavirus symptoms graphic
Image courtesy of CDC

Watu wengi walio na COVID-19 pia huhisi wamechoka sana. Dalili zingine ni: uchungu na maumivu ndani ya mwili wako, pua iliyoziba au kuchuruzika (kama homa ya mafua), kuumwa koo, kuhara, na kupoteza hisia zako za harufu.

Dalili isiyoonekana

MUHIMU: hata dalili yako ni kali, kuomba na viwango vya oksijeni yako checked. Watu wengi wenye tamaa ya tamaa-19 wana viwango vya oksijeni ya chini na hawajui. Chini ya oksijeni ngazi ni mbaya sana. Lakini kama ngazi yako ya oksijeni ni kutibiwa haraka, unaweza kupata bora zaidi kwa urahisi.

Nifanye nini ikiwa mimi ni mgonjwa?

Je, ninapaswa kupimwa kwa ugonjwa wa virusi vya corona?

Unaweza kuchukua kipimo kuona ikiwa unayo COVID-19. Mfanyakazi wa afya ataweka kijiti kidogo katika pua yako na kuchukua sampuli ya seli. Sampuli yako inapimwa katika maabara. Matokeo chanya ya kipimo yanamaanisha kuwa unayo COVID-19. Matokeo hasi ya kipimo yanamaanisha huna COVD-19.

CDC inasema kwamba sio kila mtu anahitaji kupimwa kwa COVID-19. Lakini upimaji unaweza kukusaidia kuamua nini cha kufanya ili ujitunze na kulinda watu wengine. Ikiwa una dalili na unataka kupimwa, piga simu kwa idara ya afya au daktari wako. Nenda kwenye wavuti ya CDC kupata idara ya afya katika jimbo lako.

coronavirus testing kit

Je, ikiwa sina stakabadhi halali?

Unaweza kupata huduma ya afya ikiwa hujaandikishwa lakini piga simu kabla ya kwenda kwenye kituo cha tiba. Ikiwa una dalili, piga idara ya afya ya umma kabla ya kwenda kwa daktari au kituo cha afya. Kliniki za afya na hospitali ambazo zinazosaidia wahamiaji na Wamarekani wenye kipato cha chini hazitakiwi kuripoti hali ya kisheria, na wagonjwa wanalindwa na sheria za faragha za Amerika. Unaweza kupata maelezo zaidi kwa ajili ya wahamiaji, waomba hifadhi na wakimbizi wakati wa dharura.

Je, ikiwa sina bima ya afya?

Katika jamii nyingi zilizo ndani ya nchi ya Marekani, unaweza kupata zahanati ambazo zinatoa huduma kwa wagonjwa walio na kipato cha chini na ambao hawana bima ya afya. Unaweza kutafuta huduma rahisi za matibabu katika zahanati zilzo karibu na unapoishi.

Maelezo haya ni yanatoka kwa duru za kuaminika, kama vile Kituo cha Kudhibiti Magonjwa na Shirika la Afya Duniani. USAHello halitoi ushauri wa kisheria au kimatibabu, wala rasilimali zetu hazikusudiwi kuchukuliwa kama ushauri wa kisheria au kimatibabu. Taarifa yetu ya kiafya imepitiwa na mjumbe wa bodi ya USAHelloTej Mishra, mtaalamu wa afya ya umma wa Marekani na mtaalamu wa magonjwa.

Je, una maswali mengine yeyote kuhusiana na hatua za kuchukua ukiugua? Unaweza kuuliza [email protected].