Pata kituo cha juu na habari ya wazee

Kiingereza piaKiingereza hakuna

Je wewe ni mhamiaji au mkimbizi? Je, mna mtu aliyezeeka au mzee katika familia yako? Pata habari kuhusu wazee. Tafuta kituo cha kutunza wazee na jifunze njia za kukutana na wazee katika jamii yenu.

Are you a senior immigrant or refugee? Do you have an elder in your family? Learn about resources for seniors. Find a senior center and learn other ways to meet older members of your community.

two older women - senior center

two older women - senior center

Jamii nyingi nchini Marekani ni kubwa na si kila mtu anamfahamu jirani yake. Huenda ikawa vigumu kwa wazee kukutana na wenzao waliozeeka. Pamoja na hayo, kila jamii ina vituo vya wazee.

In the USA, many communities are big, and not everyone knows their neighbors. It can be hard for older people to meet other senior citizens. But every community has a social place called a senior center.

Tazama wakimbizi wazee wanaposimulia tajriba zao

Watch refugee elders talk about their experiences

Huenda wewe pia umekumbana na mambo mengi kama watu walioonyeshwa katika video na hali hiyo imekufanya uwe imara. Hata hivyo, kuanza maisha upya katika nchi kubwa na geni huenda ikakufanya uwe mpweke. Sote katika Kituo cha Wakimbizi Mtandaoni tunafuraha sana kwamba uko nasi. Tunataka kukusaidia ukabiliane vyema na changamoto yoyote na uwe na uhusiano mzuri na wenyeji.

Like the people in the video, you have probably survived many things that have made you strong. But it can be lonely starting a new life in a big country. At USAHello, we are glad you are here. We want to help you find your way and connect with people.

Jinsi ya kupata marafiki katika eneo unaloishi

How to meet people in your neighborhood

Tembelea maktaba iliyo katika eneo lako

Use your local library

Maktaba za Marekani zina zaidi ya vitabu. Taarifa na elimu. Unaweza kujiunga na darasa la kompyuta, ukafuata na kujua matukio au maonyesho katika eneo lenu au ushauri kuhusu kazi. Maktaba nyingi zinafundisha watu kusoma na kuandika. Ikiwa katika eneo lako hakuna, maktaba hiyo inaweza kukuelekeza maeneo utakayopata mafunzo hayo.Tafuta maktaba iliyo karibu nawe

American libraries are for more than just books. They are centers for information and education. You can join a computer class, find out about local events, and get advice about jobs. Some have English classes. Many libraries have classes for people to learn to read and write. If they do not, your library can help you find classes. Find your nearest library.

Vituo vya wazee

Senior centers

Katika vituo vya wazee utapata chakula cha mchana, michezo, madarasa na mambo mengine kwa ajili ya wazee tu. Vituo hivyo vinawafaa pia wageni nchini. Vituo vya wazee hutoa huduma bure bila malipo. Unaweza kuwa katika kituo hicho siku nzima. Utahitaji kulipa kiasi kidogo tu cha pesa kwa ajili ya chakula cha mchana na matembezi ikiwa kituo kitaandaa matembezi. Hata hivyo, huduma nyingi na madarasa hutolewa bure bila malipo. Maktaba iliyo katika eneo lenu itakupa taarifa eneo utakalopata vituo vya wazee katika eneo lenu.

At the senior center, they have lunches, games, classes, and other activities just for elders. Some senior centers are even for newcomers. Senior centers are mostly free. You can go for the whole day. You may pay a small amount for lunch or for outings. But most activities and classes are free. Your local library will tell you where to find senior centers in your community.

Bustani za jumuiya

Community gardens

Ikiwa umetokea maeneo ya vijijini, huenda unakosa sana kulima au kuwa na bustani. Katika miji mikubwa bado unaweza kupata bustani ya jamii. Unaweza kusitawisha mboga, ukaisaidia jumuiya yako na kukutana na wakulima na watunza bustani wenzako.Tafuta bustani ya jumuiya

If you come from a country region, you are probably missing farming or gardening. But even in big cities, you can find a community garden. There you can grow your own vegetables, help your community, and meet other farmers and gardeners. Find a community garden.

Jinsi ya kujifunza mambo mapya

How to learn new things

Huenda ukahisi mpweke ikiwa unaishi na watu wanaozungumza lugha tofauti na yako. Je, unataka kuboresha Kiingereza chako? Ni kweli kwamba kufanya hivyo huenda kukawa changamoto kwako lakini ni jambo linalofurahisha. Na madarasa ya kufundisha Kiingereza ni njia bora ya kukutana na watu na kupata marafiki.Tafuta Katika Jiji Langu

It can be lonely if you live in a community where people do not speak your language. Do you want to improve your English? It is a challenge, but also it can be fun. And English classes are a good way to meet other people in your situation. you can search FindHello to find English classes near you. Enter your city and state. Then select Education and English classes.

ili kupata madarasa ya Kiingereza yaliyo karibu nawe. Jaza jiji unaloishi na jimbo.Kisha bofya Elimu na ESL.Unahitaji kujifunza kuongea Kiingereza kupitia mtandao Ni sawa kama usingepeda kwenda darasani au kusoma

If you do not like the idea of a class or cannot get to a class, that is okay. Instead, you can learn English conversation online.

Unaweza kujiunga pia na kozi ya bure ya uraia mtandaoni. Hata kama huna mpango kwa sasa wa kuomba kuwa raia, kujifunza kozi hii kutakusaidia kuboresha Kiingereza chako na kukufundisha kujua mambo kuhusu Marekani.

Even if you are not trying to be a citizen, you can take our free citizenship class. It will help your English and teach you about the United States.

Jitolee kusaidia wazee au watoto

Volunteer with seniors or children

Unaweza kusaidia wageni. Kutoa zawadi ya muda wako na uwepo wako kunaweza kumsaidia mzee anayehisi upweke. Ikiwa katika eneo lako kuna kituo cha kusaidia wageni kupata makazi, waulize ikiwa kuna yeyote wanayemjua anayehitaji msaada.Kutana na mzee anayejitolea kama mwandamani wa wazee

You can help other newcomers. Giving the gift of your time and company can help another senior who is lonely. Read about an elder who became a senior companion. If you have a local resettlement agency, ask if they know someone who may need your help.

Huenda una wajukuu wanaosoma shule katika eneo unaloishi. Unaweza kujitolea kufanya kazi darasani, chumba cha chakula au eneo la kuchezea watoto. Huenda kuna watoto ambao ni wageni katika eneo lako wanaohitaji msaada katika lugha yao.

You may have grandchildren in a local school. Maybe you can volunteer in the classroom, dining room, or playground. There may be newcomer children who need help in their own language.

Kutunza afya yako

Taking care of your health

Ni jambo la muhimu kwa wazee kutunza afya zao. Kuna vyanzo vingi vya kukusaidia kutunza afya nchini Marekani.

It is important for seniors to take care of their health. There are many health resources for seniors in the United States.

Kupata bima ya afya

Getting health insurance

Bima ya afya kwa wazee huitwa Huduma ya Afya. Wazee wengi (umri wa miaka 65 au zaidi) wana Huduma ya Afya. Ili upate bima hiyo lazima uwe umeishi miaka 5 nchini Marekani. Unaposubiri kupata bima hiyo, unaweza kupata bima ya afya kupitia kampuni ya bima kulingana na jimbo ulilopo.Soma zaidi kuhusu bima ya afya kwa wahamiaji wazee

Public health insurance for seniors is called Medicare. Most seniors (age 65 or older) have Medicare. But first, you must live in the United States for more than 5 years. While you are waiting to get Medicare, you can get health insurance from an insurance company through the health exchange in your state. Read more about health insurance for senior immigrants.

Hauwezi kupata bima hiyo Ikiwa hauishi kihalali (wahamiaji haramu) nchini. Pamoja na hayo, nchini Marekani kuna hospitali zinazosaidia watu wasioishi kihalali.Tafuta Katika Jiji Langu ili kupata hospitali za jumuiya zilizo karibu nawe. Jaza jiji unaloishi na jimbo. Kisha bofya Huduma ya Afya.

If you are undocumented (have no legal papers) you cannot get health insurance. But there are clinics in the United States who help undocumented immigrants. Look at FindHello to find community healthcare near you. Enter your city and state. Then select Healthcare and Mental Health.

Kumwona daktari

Going to the doctor

Unaweza kuomba kuwa na mkalimani unapopanga kumwona daktari.Jinsi ya kumwona daktari

When you make an appointment with a doctor, you can ask for an interpreter. Find out how to go to the doctor.

Mazoezi

Fitness

Jambo moja unaloweza kufanya ili kuwa na afya bora na kupata marafiki ni kujiunga na darasa la kufanya mazoezi ya mwili! Uliza wahusika katika kituo cha wazee karibu nawe, kituo cha jumuiya au maktaba kuhusu madarasa ya kufanya mazoezi ya mwili ya wazee.

One of the best things you can do to stay healthy and meet people is to join an exercise class! Ask at your senior center, community center, or library about exercise classes for your age group.

Equipped wanayopata wazee

Public benefits for seniors

Ukiwa mkimbizi au mkazi wa Marekani, unastahili kunufaika na mfuko wa jamii. Manufaa hayo yanatia ndani kwa walemavu, wasio na kazi au wazee Fahamu kuhusu manufaa ya mfuko wa jamii

As a refugee or other US resident, you can qualify for public benefits. These include benefits for people who are disabled, unemployed or over a certain age. Learn more about public benefits.

Nyongeza ya Mapato (SSI) imewekwa kusaidia watu wazima walemavu, watoto na watu wenye umri wa miaka zaidi ya 65 wenye kipato kidogo. Baadhi ya wasio raia wanaweza kupata SSI.Pata habari kuhusu SSI kwa wasio raia

Supplemental Security Income (SSI) is to help disabled adults, children, and people over 65 who have low income. Some non-citizens can receive SSI. Learn about SSI for non-citizens.

Taarifa muhimu kuhusu SSI:Baadhi ya wakimbizi au watu wasio raia wanaopata SSI hawataendelea kupata baada ya miaka 7.Hata hivyo utaendelea kupata SSI kwa kadiri utakavyohitaji ukiwa raia.Jinsi ya kuwa raia wa Marekani

An important note about SSI: Some refugees and other non-citizens who get SSI will stop getting it after 7 years. But if you become a citizen, you can continue to receive SSI for as long as you need it. Learn how to become a US citizen.

Msaada wa kisheria na dharura

Legal and emergency help

Wazee wengi hunyanyaswa (kuumizwa) na kutapeliwa (kudanganywa). Ikiwa unanyanyaswa nyumbani au unahisi kwamba kuna mtu anayekutapeli, toa taarifa mara moja kwa daktari wako, polisi au mhusika katika kituo cha wazee unachohudhuria. Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kukunyanyasa hata kama ni ndugu yako.Kupata msaada au kutoa taarifa ikiwa unanyanyaswa, anza hapa na chagua jimbo lako Baada ya kuchagua jimbo lako, utaona namba ya simu ya kupiga karibu na ramani.

Many older people suffer from abuse (being hurt) and fraud (being cheated). You can tell your doctor, the police, or someone at your senior center if you are being mistreated at home or if you think someone is cheating you. Nobody is allowed to hurt you, even if they are in your own family. To get help or report abuse, go to the NAPSA website and choose your state. After you choose your state, you will find a phone number to call next to the map.

Ikiwa unahitaji mwanasheria, unaweza kupata msaada wa kisheria. Jaza jiji unaloishi na jimbo. Kisha bofya Haki na Sheria. Huduma nyingi zilizoorodheshwa zinaweza kukusaidia katika lugha yako. FindHello

If you need a lawyer, you can find legal help. Enter your city and state. Then click Rights and Laws. Many of the services listed can help you in your own language. You can search for lawyers with FindHello. Enter your city and state. Then select Citizenship and Immigration.

Unataka taarifa zaidi?

Do you need more information?

Ikiwa hujapata unachotafuta katika ukurasa huu, tafadhali usikate tamaa! Badala yake muulize mhusika katika kituo cha wazee unachoshirikiana nacho, wakala wa wahamiaji au maktaba. Kazi yao ni kukusaidia kupata unachotafuta. Unaweza kutumia mtandao kupata msaada pia.

If you do not find what you are looking for on this page, please do not give up! Instead, ask at your senior center, resettlement agency, or library. Their job is to help you find what you need. You can use the internet to help you, too.

Tafuta kwenye wavuti

Search on the internet

Hapa kuna maneno kadhaa ya Kiingereza ambayo yatakusaidia kutazama kwenye wavuti:

Here some English words that will help you to look on the internet:

  • tafuta kituo cha kutunza wazee….(weka jina la jiji lako)
  • tafuta taarifa kwa ajili ya wazee….(weka jina la jiji lako)
  • find a senior center in … (add the name of your city)
  • find resources for seniors in … (add the name of your city)

Pata msaada wa tafsiri

Get help with translation

Ikiwa unashindwa kufanya utafiti kwa kutumia Kiingereza, tumia kifaa cha kutafsiri. Unaweza kuandika maneno katika Google Translate na itakuambia jinsi ya kusema katika Kiingereza. Tafuta na pata msaada wa bure wa tafsiri na wakalimani

If you have trouble asking in English, use a translation tool. You can type words into Google Translate and it will tell you what to say in English. Or, you can find free translation help and interpreters.

Jifunze zaidi

Learn more

Maelezo zaidi

More information

Find help near you

Use FindHello to search for services and resources in your city.

Anza utafutizi wako

Ukurasa huu alimsaidia wewe? Uso Unaocheka Ndio Frown uso La
Asante kwa maoni yako!