Gawanya

Maswali na majibu ya mtihani wa Uraia wa Marekani

Wakati wa usaili wako wa uraia, utalazimika kufanya mtihani wa uraia wa Marekani. Pata orodha kamili ya maswali na majibu ya mtihani wa uraia katika lugha 17 tofauti. Pia kuna video zenye sauti za kukusaidia kusoma.


Mtihani wa uraia

Uraia ni mchakato ambao mkazi halali wa kudumu anakuwa raia wa Marekani. Mchakato huo unajumuisha usaili wa uraia katika Huduma za Uraia na Uhamiaji za Marekani (USCIS). Mtihani wa uraia, unaojulikana pia kama ‘civics test’, ni sehemu ya usaili huo.

Mtihani wa raia unahakikisha kuwa unaielewa serikali ya Marekani na kujua historia yake. Utalazimika kufaulu ili uwe raia wa Marekani.

(https://www.youtube.com/watch?v=cV8IcSsd3Zw)

Maswali 100 na majibu ya mtihani wa Uraia

Afisa wa USCIS atakuuliza hadi maswali 10 ya uraia. Lazima ujibu kwa usahihi maswali 6 ili ufaulu sehemu hii ya mtihani. Pata orodha kamili ya maswali na majibu haya katika lugha yako na kwa Kiingereza. Video zinaweza kukusaidia kufanya mazoezi ya majibu kwa Kiingereza.

LughaMaswali 100 na majibuVideo
Kiarabu (العربية)-KiingerezaTazama au pakua PDF Tazama video
Kichina (简体中文)-KiingerezaTazama au pakua PDF 
Kifaransa (Français)-KiingerezaTazama au pakua PDF Tazama video
Kihindi (हिन्दी)-KiingerezaTazama au pakua PDF  
Kijapani (日本語)-KiingerezaTazama au pakua PDF  
Kikareni (ကညီကျိၥ်)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kikorea (한국어)-KiingerezaTazama au pakua PDF Tazama video
Kinepali (नेपाली)-KiingerezaTazama au pakua PDF  
Kipashto (پښتو)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kiajemi (فارسی/دری)-KiingerezaTazama au pakua PDFTazama video
Kipolishi (polski)-KiingerezaTazama au pakua PDF  
Kispaniola (Español)-KiingerezaTazama au pakua PDFTazama video
Kiswahili -KiingerezaTazama au pakua PDF 
Kitagalogi -KiingerezaTazama au pakua PDFTazama video
Kithai (ภาษาไทย)-KiingerezaTazama au pakua PDF 
Kiurdu (اُردُو)-KiingerezaTazama au pakua PDF  
Kivietinamu (Tiếng Việt)-KiingerezaTazama au pakua PDF 

Jinsi ya kujibu maswali ya mtihani wa uraia

Majibu ya maswali yapo chini ya kila swali na yamewekewa alama ya nukta kubwa kwenye PDF.

Baadhi ya maswali yana jibu sahihi zaidi ya moja.

Ikiwa swali linauliza tu jibu mojawapo, unaweza kuchagua ni jibu gani utakalompa afisa wa USCIS. Hii inamaanisha unahitaji tu kujifunza jibu moja kwa maswali haya.

Maswali mengine yanaweza kuhitaji jibu zaidi ya moja.

Si lazima useme maneno kwenye mabano ( ) isipokuwa ukitaka kufanya hivyo.

Baadhi ya majibu yanaweza kubadilika.

Unaweza kuulizwa jina la afisa aliyechaguliwa. Kwa mfano, “Jina la Spika wa Baraza la Wawakilishi ni nani?” Jina linaweza kuwa limebadilika kufikia muda wa mtihani ikiwa mtu mpya amechaguliwa.

Baadhi ya majibu ni tofauti kulingana na mahali unapoishi.

Baadhi ya maswali yanahusu jimbo lako tu. Kwa mfano, “Gavana wa jimbo lako ni nani kwa sasa?”

Baadhi ya maswali yanaweza kubadilika kulingana na tarehe na mahali unapoishi. Kabla ya mtihani, angalia Ukurasa wa sasisho za mtihani wa USCIS kwa jibu sahihi.

Mtihani wa uraia kwa wenye miaka 65 na zaidi

Unaweza kufanya toleo tofauti la mtihani ikiwa una miaka 65 au zaidi na umekuwa mkazi wa kudumu (mwenye Green Card) kwa angalau miaka 20. Huu unaitwa msamaha wa 65/20.

Unahitaji tu kujifunza maswali 20 kwa ajili ya mtihani huu. Maswali 20 yametoka kwenye orodha kamili ya maswali 100. Ni yaliyowekewa alama ya nyota (*). Bado unapaswa kupata kwa usahihi maswali 6 kati ya 10 ili ufaulu mtihani. Toleo hili linaweza kufanywa kwa Kiingereza au lugha uipendayo.

LughaMaswali 20 na majibu
Kiarabu (العربية)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kichina (简体中文)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kifaransa (Français)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kihindi (हिन्दी)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kijapani (日本語)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kikareni (ကညီကျိၥ်)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kikorea (한국어)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kinepali (नेपाली)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kipashto (پښتو)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kiajemi (فارسی/دری)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kipolishi (polski)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kispaniola (Español)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kiswahili -KiingerezaTazama au pakua PDF
Kitagalogi -KiingerezaTazama au pakua PDF
Kithai (ภาษาไทย)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kiurdu (اُردُو)-KiingerezaTazama au pakua PDF
Kivietinamu (Tiếng Việt)-KiingerezaTazama au pakua PDF

Kufanya mtihani wa uraia kwa lugha nyingine

Unaweza kufanya mtihani wa uraia katika lugha yako ikiwa tu unakidhi mojawapo ya matakwa haya:

  1. Una miaka 50 au zaidi na umekuwa mkazi wa kudumu (mwenye Green Card) kwa angalau miaka 20. Huu unaitwa msamaha wa 50/20. 
  2. Una miaka 55 au zaidi na umekuwa mkazi wa kudumu (mwenye Green Card) kwa angalau miaka 15. Huu unaitwa msamaha wa 55/15.

Pata maelezo zaidi kuhusu misamaha na mazingatio kwa ajili ya usaili wa uraia.

woman waving at citizenship ceremony
Free U.S. Citizenship Class

Take USAHello’s free online class to help you prepare for the naturalization interview civics test. Available in English, Arabic, French, Spanish, Swahili, and Vietnamese.

Start the class

Mbele: Fahamu nini cha kutarajia kwenye hafla ya kiapo


Taarifa kwenye ukurasa huu umetoka kwa USCIS, USA.gov, na vyanzo vingine vinavyoaminika. Malengo yetu ni kutoa taarifa zilizo rahisi kuelewa na zinazosasishwa mara kwa mara. Taarifa hii si ushauri wa kisheria.

Share