Gawanya

Ni nini mpango wa ufadhili wa kibinafsi wa wakimbizi?

Mpango wa ufadhili wa kibinafsi Marekani unaitwa Welcome Corps. Ni mpango wa Idara ya Nchi ya Marekani unaowaruhusu raia wa Marekani na wakazi wa kudumu kuwafadhili wakimbizi kwa hiari yao. Wafadhili wanaweza kuwapatia wakimbizi usaidizi muhimu ili kuanza maisha mapya nchini Marekani. Jifunze kuhusu mchakato na mahitaji.

Imesasishwa Febuari 1, 2024

Ufadhili ni nini?

Ufadhili unamaanisha msaada unaotolewa kwa wakimbizi kwa ajili ya maakazi mapya katika nchi mpya. Wakimbizi wanaweza kupata msaada huu kupitia mashirika ya makazi au ufadhili wa kibinafsi kupitia Welcome Corps.

Makazi ya jadi ya wakimbizi yanahusisha usaidizi wa moja kwa moja kutoka serikali. Serikali inachukua jukumu la kutoa msaada wa kifedha, nyumba, na huduma nyingine muhimu kupitia mashirika ya makazi.

Ufadhili wa kibinafsi unahusisha makundi kutoka jamii ambayo kwa hiari yanachukua jukumu la kusaidia wakimbizi. Nchini Marekani, hii ni sehemu ya Welcome Corps. Wafadhili wa kibinafsi husaidia wakimbizi kutafuta nyumba, kuwapa msaada wa kifedha, na kuwasaidia wakimbizi kujumuika katika jamii.

Ni nini aina za ufadhili wa kibinafsi?

Kuna aina mbili za ufadhili kupitia Welcome Corps:

  • Ufadhili wa kulingana: Makundi ya wafadhili wanapewa mkimbizi au familia iliyoidhinishwa kwa makazi, bila ya wao kujuana binafsi awali.
  • Ufadhili wa kutaja jina: Makundi ya wafadhili yanachagua kusaidia mkimbizi au familia mahususi ambayo tayari wanaijua binafsi.
Ufadhili wa kibinafsi ni kupitia kundi la washirika watano linaloitwa kundi la wafadhili wa kibinafsi (PSG). Shirika linalosaidia makundi ya wafadhili linaitwa shirika la wafadhili wa kibinafsi (PSO). Ni muhimu kutambua kwamba mashirika haya hayawezi kukufadhili.

Taarifa kwa wale wanaotaka ufadhili

Je, ni mahitaji gani ya kufadhiliwa?

Welcome Corps hutoa chombo cha kustahiki ambacho kinaweza kukusaidia kujua ikiwa unaweza kuwa katika mpango huu.

Ili kufadhiliwa na mtu unayemjua na kuja Marekani, unapaswa:

  • Kuwa umesajiliwa kama mkimbizi na UNHCR au serikali yako ya kienyeji ya sasa mnamo au kabla ya tarehe 30 Septemba, 2023. Ikiwa uko mkimbizi kutoka Cuba, Haiti, Nicaragua, au Venezuela, Fomu I-134 inapaswa kuwa imewasilishwa kwa niaba yako kabla ya tarehe 30, Septemba, 2023. Ni lazima uwe umekuwa nje ya nchi yako ya utaifa wakati fomu ilipoawasilishwa.
  • Kuwa sasa unaishi nje yako ya nyumbani katika taifa linaloidhinishwa kwa ajili ya mchakato wa ufadhili.
  • Kwa sasa unaishi nje ya nchi ya Marekani.
  • Kuwa na umri wa miaka zaidi ya 18, au kuchakatwa pamoja na mzazi au mlinzi wa kisheria. Watoto ambao hawasindikizwi hawastahiki. 
  • Kukamilisha mahojiano yote yanayotakiwa, uchunguzi, na michakato ya ukaguzi. 
  • Kuidhinishwa kwa makazi mapya nchini Marekani na serikali ya Marekani.
Kwa mujibu wa sheria ya Marekani, mkimbizi ni mtu aliyelazimika kuondoka nchi yake ya nyumbani kwa sababu maisha yake yako hatarini kwa sababu ya rangi yake, dini, utaifa, maoni yake ya kisiasa, au kuwa mojawapo wa kundi fulani la kijamii. 

Hakuna mahitaji ya utaifa. Unaweza kuwa unatoka nchi yoyote ili kufadhiliwa.

Ni nani asiyestahiki?

Watu ambao hawafikii vigezo au wanaoishi katika nchi fulani hawastahiki kwa wakati huu.

  • Hustahiki kufadhiliwa na mtu unayemjua ikiwa umejisajili kwa hali ya mkimbizi baada ya tarehe 30 Septemba, 2023. Unapaswa kuwa tayari mkimbizi uliyesajiliwa katika nchi nyingine kabla ya tarehe hii ili kustahiki. Baadhi ya watu sasa wanahamia katika nchi tofauti ili kujiandikisha kwa mpango huu. Usihamie katika nchi tofauti ili kustahiki kwa mpango. Welcome Corps haitakubali ombi kwa niaba yako.
  • Wakimbizi wanaoishi katika nchi fulani hawastahiki kwa ufadhili wa kibinafsi. Kuna sababu nyingi zinazowezekana kwa hili. Wakimbizi kutoka moja ya nchi hizi wanaweza kustahiki ikiwa hawaishi hapo kwa sasa.  Angalia orodha ya nchi hizi hapa.
  • Watoto wadogo wasiosindikizwa hawastahiki kwa ufadhili wa kibinafsi. Watoto wote walio chini ya umri wa miaka 18 wanapaswa kufadhiliwa pamoja na mzazi wao au mlezi wa kisheria. Sheria hii ipo ili kuwalinda watoto.
Onyo: Kushiriki katika Mpango wa Marekani wa Kupokea Wakimbizi, ikiwemo kupitia Welcome Corps, siku zote ni bure. Hupaswi kulipa pesa ili kutuma ombi kwa mpango huu. Mtu anapokuambia kwamba anaweza kukuingiza kwenye mpango ikiwa unampatia pesa au upendeleo, ni ulaghai. Ripoti mtu yeyote binafsi au kundi linalofanya hivi kwa [email protected]

Ni jinsi gani ninapata mfadhili wa kibinafsi?

Kwa wakimbizi, kupata mfadhili wa kibinafsi siyo mchakato wa moja kwa moja. Ili kulinganishwa na mfadhili usiyemjua, unahitaji kwanza kuidhinishwa kwa ajili ya makazi mapya nchini Marekani kupitia Mpango wa Marekani wa Kupokea Wakimbizi. Ikiwa unaidhinishwa kufadhiliwa, utafahamishwa na mfanyakazi katika Kituo chako cha Usaidizi cha Makazi Mapya

Hakuna mtu anayeweza kukuhakishia au kukusaidia kupata kiingio maalum katika mpango. Wakimbizi wote ni lazima wapitie Mpango wa Marekani wa Kupokea Wakimbizi na kuidhinishwa na serikali ya Marekani.

Je, mtu ninayemjua anaweza kunifadhili?

Ndiyo, lakini mfadhili wako ni lazima aombe hivyo. Ikiwa unajua mtu nchini Marekani anayetaka kukufadhili, anaweza kutuma ombi la kukufadhili kupitia rufaa. Anapaswa kukidhi mahitaji ya kuomba ili kuwa kundi la wafadhili. Anahitaji kutoa habari kuhusu wanafamilia wote katika ombi lake. Maelezo haya yatatumiwa na serikali ya Marekani ili kuamua kuhusu kesi yako ya ukimbizi.  Yajue mengi zaidi.

Ninaweza kutegemea nini ikiwa ninafadhiliwa?

Kama mkimbizi anayefadhiliwa nchini Marekani, utapata usaidizi katika kupata pahali pa kuishi na vitu vya msingi unavyohitaji. Unaweza pia kupata msaada na mafaa ya serikali. Hivi ni pamoja na huduma za afya, elimu ya watoto wako, kukusaidia kutafuta kazi, na huduma nyingine ili kurahisisha zaidi ukaaji.

Wakimbizi wanaofadhiliwa hawatakuja nchini Marekani kwa haraka zaidi kuliko wakimbizi waliopewa makazi mapya katika mchakato wa umma. Wakimbizi wote wanaoingia nchini Marekani wanapitia mahitaji sawa ya usindikaji.

Ni mipango gani mingine ya ufadhili?

Mipango mingine ya ufadhili inayopatikana ni:

Mipango hii miwili ina sheria tofauti na zile zilizoorodheshwa kwenye ukurasa huu.

Taarifa kwa wafadhili nchini Marekani.

Ni nini mahitaji ya kuwa mfadhili wa kibinafsi?

Ili kuwa mfadhili wa kibinafsi, unapaswa:

  1. Kuwa raia wa Marekani au mkaaji wa kudumu.
  2. Kuunda kundi la angalau washiriki watano.
  3. Kuishi karibu na pahali mkimbizi atakapopewa makazi mapya.
  4. Kukamilisha ukaguzi wa usuli na kukubali kanuni za maadili.
  5. Kutoa mpango wa kina wa msaada kwa mkimbizi.

Ni vipi ninaweza kuwa mfadhili wa kibinafsi?

Tuma ombi kupitia Welcome Corps. Utahitaji kuunda kundi la wahifadhi na kutimiza mahitaji fulani kama ukaguzi wa usuli na kuandaa mpango wa msaada kwa mkimbizi. 

Wfadhili wanaweza kuwasilisha ombi moja tu kwa wakati mmoja. Ombi moja linaweza kuwa kwa mtu binafsi au familia.

Je, ninaweza kuomba kufadhili mtu mahususi?

Ndiyo, unaweza kuchagua kufadhili mkimbizi au familia ya mkimbizi mahususi ambayo unaijua tayari. Unapaswa kutuma ombi  kwa Welcome Corps kwa rufaa na kutoa taarifa kuhusu mtu unayetaka kumfadhili.

Usalama

Welcome Corps ina hatua nyingi za kuhakikisha kwamba mchakato uko salama. Wafadhili wa kibinafsi wana ukaguzi wa usuli na wanapaswa kufuata kanuni kali za maadili. Wakimbizi hupitia taratibu rasmi nyingi za ukaguzi ikiwemo mahojiano ya kina, uchunguzi wa kiusalama unaofanywa na mashirika ya Marekani na ukaguzi wa afya.

Wakimbizi wanapaswa kujua kwamba hawatakiwi kulipa, kufanyia kazi, au kusogea karibu mtu yeyote ili kufikia mpango. Maombi yoyote kama hayo yanapaswa kuripotiwa wakati huo huo kwa Welcome Corps kwa [email protected].

Thank you to our partner Tarjimly for help translating this page


Taarifa kwenye ukurasa huu umetoka kwa Welcome Corps, Community Sponsorship Hub, ECDC, na vyanzo vingine vinavyoaminika. Malengo yetu ni kutoa taarifa zilizo rahisi kuelewa na zinazosasishwa mara kwa mara. Taarifa hii si ushauri wa kisheria.

Share