Mafao ya wahamiaji na huduma za wakimbizi

Imerekebishwa Juni 12, 2024
Je, unapata wakati mgumu kulipia gharama za msingi za maisha? Mafao na huduma za serikali kutoka kwa serikali ya Marekani yanaweza kusaidia. Fahamu kuhusu machaguo ya wahamiaji na wakimbizi na jinsi ya kuomba. 

Kumbuka: Sera za uhamiaji za Marekani zinabadilika chini ya utawala wa Trump. Baadhi ya taarifa za hapa chini zinaweza kuwa zimepitwa na wakati. Pata maelezo kuhusu mabadiliko ya sasa hapa.

Mafao ya serikali ni nini?

Serikali ya Marekani inatoa ruzuku ya serikali kwa huduma muhimu, ikiwemo chakula, makazi, huduma za afya, na elimu. Mashirika ya huduma za kijamii hutoa mipango hii ya serikali kuu. Wao husaidia:

  • Watu wenye kipato cha chini
  • Watu wasio na makazi
  • Watu wenye ulemavu

Ruzuku nyingi za serikali hutegemea mapato yako na ukubwa wa familia. Zinakusudiwa kukusaidia kwa muda. Kiasi cha msaada unachopata kinaweza kupungua au kusitishwa mara tu unapopata kipato kikubwa zaidi.

Kila jimbo linaendesha mpango wake binafsi, hivyo ruzuku ya serikali zinaweza kutofautiana kutoka jimbo moja hadi jingine. Ukihama, kwa kawaida utapaswa kuomba tena msaada katika jimbo lako jipya.

Wakimbizi, watafuta hifadhi, na wahamiaji wengine wanaweza pia kustahiki kupata huduma za ziada zinazotolewa na Ofisi ya Makazi ya Wakimbizi (ORR).

Nani anaweza kupata ruzuku za serikali?

Raia wa Marekani na wahamiaji wenye sifa wanastahiki kupokea ruzuku ya serikali. Wahamiaji wenye sifa ni pamoja na:

  • Wakazi halali wa kudumu (Wamiliki wa Green Card)
  • Wakimbizi na Waomba Hifadhi
  • Wahamiaji kutoka Cuba na Haiti
  • Wamiliki wa Visa Maalum ya Wahamiaji
  • Waathirika wa usafirishaji haramu wa binadamu
  • Parole ya kibinadamu

Kustahiki pia kunategemea masharti maalum ya kila jimbo. Kila jimbo lina sheria zake. Baadhi ya majimbo yanatoa mafao ya umma kama vile bima ya afya kwa wakazi wote, bila kujali hali ya uhamiaji.

Wahamiaji wasio na vibali na wengine ambao hawajaorodheshwa kwa ujumla hawastahili kupata ruzuku ya serikali. Hata hivyo, wanaweza kupata msaada kutoka kwenye mashirika ya huduma za kijamii ya eneo na mipango ya jamii.

Shirika la huduma za kijamii la eneo lako linaweza kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo. Benefits.gov inaorodhesha ruzuku kulingana na kila jimbo.

Ni aina gani za ruzuku za serikali?

Msaada wa Muda kwa Familia zenye Uhitaji (TANF)

TANF (pia inaitwa msaada wa kijamii) hutoa fedha kwa familia zenye kipato cha chini. Mpango huo unasaidia kulipia gharama za chakula, makazi, utunzaji wa watoto, na mafunzo ya kazi. Utapokea manufaa ya TANF kupitia kadi ya benki, amana ya moja kwa moja, au hundi za karatasi kulingana na jimbo lako.

Ni muhimu kujua kwamba kiasi cha msaada unachopokea kinaweza kuwa tofauti sana na cha mtu aliye katika jimbo tofauti. Kila jimbo lina kiasi chake kinachotegemea ukubwa wa kaya na mapato.

Jinsi ya kuomba: Wasiliana na mpango wako wa TANF wa eneo lako kwa taarifa kuhusu vigezo vya ustahiki na jinsi ya kuomba.

Kipato cha Usalama wa Ziada (SSI)

SSI inatoa malipo ya kila mwezi kwa watu wazima wenye umri wa miaka 65 au zaidi ambao wamestaafu na hawafanyi kazi tena, au wanaopata kiasi kidogo kila mwezi. Kiasi cha malipo ya kila mwezi kinaweza kubadilika kulingana na mapato, rasilimali, na hali yako ya maisha.

Tafuta taarifa za SSI katika lugha mbalimbali.

Jinsi ya kuomba: Jaza fomu ya maombi mtandaoni. Unaweza pia kupiga simu kwa laini ya msaada ya SSI kwa 1-800-772-1213. Utapokea miadi ya kukamilisha ombi lako.

Bima ya Ulemavu ya Hifadhi ya Jamii (SSDI)

SSDI inatoa mapato kwa watu wenye ulemavu ambao unawazuia au unapunguza uwezo wao wa kufanya kazi kwa mwaka mmoja au zaidi. Malipo yako ya kila mwezi yanategemea historia yako ya kazi. Pia, utapata bima ya afya kupitia Medicare.

Medicaid

Medicaid inatoa bima ya afya ya bila malipo au ya gharama nafuu kwa wazee, watu wenye ulemavu, watoto, wanawake wajawazito, na familia zenye kipato cha chini. Wahamiaji wengi wanapaswa kusubiri miaka 5 baada ya kupokea hadhi ya uhamiaji kabla ya kuomba Medicaid. Wakimbizi na Waomba Hifadhi hawana haja ya kusubiri.

Medicaid ya Dharura hulipia huduma za dharura, ikiwa ni pamoja na kuwa hospitalini. Medicaid ya dharura inapatikana kwa wahamiaji ambao hawachukuliwi kuwa “wasio raia wenye sifa” lakini wanakidhi kanuni zote za kipato na makazi ya jimbo. Wahamiaji wasio na vibali wanaweza kuomba Medicaid ya Dharura.

Jinsi ya kutuma maombi: Jaza fomu ya maombi na Soko la Bima ya Afya. Unaweza pia kuangalia shirika la Medicaid la jimbo lako kwa taarifa kuhusu ustahiki na jinsi ya kuomba.

Pata maelezo zaidi kuhusu ruzuku kwa watu wenye ulemavu.

Mpango wa Bima ya Afya ya Watoto (CHIP)

Mpango wa Bima ya Afya ya Watoto (CHIP) inatoa bima ya afya ya bila malipo au ya gharama nafuu kwa watoto na wanawake wajawazito. Hii ni kwa familia ambazo zinapata kipato kikubwa kiasi cha kutostahiki Medicaid. Katika baadhi ya majimbo, unapaswa kusubiri miaka 5 baada ya kupata hadhi ya uhamiaji kabla ya kujiandikisha katika CHIP.

Jinsi ya kutuma maombi: Jaza fomu ya maombi kwenye Soko la Bima ya Afya. Pata taarifa zaidi kuhusu mpango wa CHIP katika jimbo lako.

Medicare

Medicare inatoa bima ya afya ya bila malipo au ya bei nafuu kwa watu wazima wenye umri wa miaka 65 au zaidi na watu wenye ulemavu na magonjwa makubwa.

Jinsi ya kuomba: Jaza ombi la mtandaoni la Medicare. Unaweza kujiandikisha kwenye Medicare unapojiunga na ruzuku za Hifadhi ya Jamii au unapostaafu. Piga simu kwenye namba ya Medicare kwa 1-800-633-4227 ili kupata msaada katika lugha yako.

Mpango Msaada wa Lishe ya Ziada (SNAP)

SNAP (food stamps) husaidia familia zenye kipato cha chini kununua chakula kwa kutumia kadi. Utapokea ruzuku ya SNAP kwenye kadi ya Electronic Benefits Transfer (EBT). Inafanya kazi kama kadi ya benki.

Kila mwezi, unapokea kiasi fulani cha pesa kwenye kadi yako. Unaweza kutumia kadi kununua bidhaa za vyakula katika maduka yaliyoidhinishwa. Lazima ukidhi vigezo fulani vya mapato na kazi ili ustahiki kupata SNAP.

Ikiwa wewe si raia wa Marekani, lazima pia utimize angalau moja kati ya yafuatayo ili kuwa na sifa:

  • Umeishi Marekani kwa zaidi ya miaka 5
  • Unapata ruzuku zinazohusiana na ulemavu
  • Lazima uwe umri wa chini ya miaka 18

Jinsi ya kuomba: Wasiliana na ofisi ya SNAP katika jimbo lako kwa taarifa kuhusu jinsi ya kuomba.

Ikiwa hustahili kupata SNAP au haikidhi mahitaji yako, vituo vya chakula hutoa vyakula vya bila malipo na kwa kawaida hupatikana kwa yeyote anayehitaji.

Mpango Maalum wa Lishe ya Ziada kwa Wanawake, Watoto Wachanga na Watoto Wadogo(WIC)

WIC inasaidia wanawake wajawazito na wanaonyonyesha pamoja na watoto walio chini ya miaka 5 kupata chakula, ushauri wa lishe, na kuelekezwa kwenye huduma za kijamii. Lazima ukidhi vigezo fulani vya mapato na afya ili kustahiki.

Jinsi ya kuomba: Wasiliana na shirika la WIC la jimbo lako au eneo lako kwa maelezo kuhusu jinsi ya kuomba.

Msaada wa chakula kwa wazee

Baadhi ya majimbo hutoa msaada wa chakula kwa watu wazima wenye umri wa miaka 60 au zaidi ambao wana kipato cha chini kupitia Mpango wa Lishe wa Soko la Wakulima Wakubwa na Mpango wa Chakula cha Ziada. Mipango hii ya msaada inajumuisha vifurushi vya kila mwezi vya chakula bora na kuponi za kununua vyakula kwenye masoko ya wakulima. Wazee wanaweza pia kustahiki kupata msaada wa chakula kutoka SNAP.

Jinsi ya kuomba: Wasiliana na mpango wa chakula na lishe katika jimbo lako kwa taarifa kuhusu jinsi ya kuomba.

Vyakula vya bila malipo au vya bei nafuu shuleni

Shule hutoa chakula cha bila malipo au kwa gharama nafuu wakati wa mwaka wa shule na wakati wa mapumziko ya majira ya joto. Watoto wako wanaweza kustahiki kulingana na mapato ya kaya yako. Ikiwa unapokea ruzuku ya SNAP au TANF, watoto wako watastahili moja kwa moja kupata chakula cha bila malipo shuleni.

Jinsi ya kuomba: Shule kwa kawaida hutuma fomu za maombi nyumbani mwanzoni mwa mwaka wa shule. Unaweza pia kuomba fomu ya maombi kwenye ofisi ya shule yako wakati wowote katika mwaka wa masomo.

Nyumba za serikali na vocha

Serikali ya Marekani inatoa makazi ya serikali au yenye ruzuku kwa familia zenye kipato cha chini, wazee, na watu wenye ulemavu. Fleti hizi kwa kawaida zina kodi iliyopunguzwa. Unaweza pia kuomba vocha za kulipia kiasi au kodi yako yote.

Jinsi ya kuomba: Wasiliana na shirika la makazi ya serikali katika jimbo lako kwa taarifa zaidi.

Pata taarifa zaidi kuhusu makazi kwa wahamiaji.

Msaada wa kulipa bili za huduma

Mpango wa LIHEAP husaidia watu wenye kipato cha chini kulipia gharama za nishati za nyumbani, kama vile gesi na umeme.

Jinsi ya kuomba: Wasiliana na ofisi ya LIHEAP katika jimbo lako kwa taarifa zaidi.

Mpango wa WAP husaidia kulipia maboresho ya nyumbani yanayookoa pesa kwenye bili za nishati.

Jinsi ya kuomba: Wasiliana na ofisi ya WAP katika jimbo lako kwa taarifa zaidi.

Lifeline huwasaidia watu wenye kipato cha chini kulipia huduma za simu na intaneti.

Jinsi ya kuomba: Wasiliana na kampuni yako ya simu au intaneti ili kujiandikisha kwa huduma ya Lifeline.

Je, mnufaika wa ruzuku za serikali nini?

Mnufaika wa ruzuku za serikali ni mtu ambaye maafisa wa uhamiaji wanaamini atateigemea serikali kwa ajili ya fedha na msaada. Ikiwa unachukuliwa kuwa mnufaika wa ruzuku za serrikali, huenda usiweze kuomba hadhi ya uhamiaji.

Ruzuku 2 tu za serikali zinazohesabiwa kwa mnufaika wa ruzuku za serikali:

  1. Msaada wa kifedha wa serikali (ikiwemo SSI na TANF)
  2. Huduma ya muda mrefu (kupitia Medicaid au mpango mwingine)

Msaada wa serikali hauhusiki na vikundi vinavyostahiki kupata huduma za ORR, ikiwemo wakimbizi na waomba hifadhi. Pata maelezo zaidi kuhusu kanuni ya msaada wa serikali.

Ruzuku na huduma za ORR ni ninii?

Ruzuku za muda mfupi

Ruzuku na huduma za ORR huwasaidia wakimbizi, waomba hifadhi, na wahamiaji wengine wapya kulipia mahitaji ya msingi wanapolowea Marekani. Serikali za majimbo, mashirika ya makazi mapya ya eneo husika, na mashirika ya jamii hutoa huduma hizi. Tafuta taarifa za ORR katika lugha mbalimbali.

Ruzuku za ORR zinapatikana kwa makundi haya:

  • Wakimbizi na Waomba Hifadhi
  • Parole za Afghanistan na Ukraine
  • Wamiliki wa SIV ya Afghanstani na Iraq
  • Wahamiaji kutoka Cuba na Haiti
  • Waathirika wa usafirishaji haramu wa binadamu
  • Manusura wa mateso
  • Waasia-Wamarekani

Ruzuku za muda mfupi

Ruzuku za ORR na huduma nyingi zinapatikana kwa muda wa miezi 12 baada ya kuwasiri Marekani.

Jinsi ya kuomba: Jisajili na shirika lako la makazi mapya ya wakimbizi mara tu unapopata hadhi yako. Kama wewe ni mkimbizi, utaunganishwa moja kwa moja na shirika la makazi mapya. Watakusaidia kujiandikisha katika mipango hii. Zungumza na mfanyakazi wako wa kesi kama una maswali yoyote.

Ruzuku za muda mfupi ni pamoja na:

Msaada wa fedha taslimu kwa wakimbizi (RCA)

Ikiwa hustahili SSI au TANF, unaweza kupata hadi miezi 12 ya msaada wa pesa taslimu. Unaweza kutumia RCA ili kukusaidia kulipia chakula, makazi, na usafiri.

Unaweza pia kupata mipango ya kujitosheleza na huduma za ajira kupitia mpango huu.

Mpango wa ruzuku ya kufanana (MG)

Unaweza kuchagua kujiandikisha katika mpango wa MG badala ya RCA. MG inatoa msaada wa pesa, upangaji wa bajeti ya familia, usimamizi wa kesi, na huduma za ajira kwa muda wa hadi miezi 8 (siku 240).

Mpango huo pia unatoa msaada wa makazi, usafiri, afya, na mafunzo ya lugha ya Kiingereza.

Msaada wa matibabu kwa wakimbizi (RMA)

Ikiwa haustahiki Medicaid, unaweza kupata hadi miezi 12 ya RMA. RMA inatoa bima ya afya ya bure au ya gharama nafuu sawa na Medicaid. Unaweza kuomba bima ya matibabu kupitia soko la bima ya afya baada ya RMA kumalizika.

Unaweza kufanyiwa uchunguzi wa bure wa afya katika idara ya afya ya eneo lako baada ya kuwasili Marekani. Itajumuisha chanjo zozote zinazohitajika. Mtoa huduma za afya atakuelekeza kwa daktari wa huduma ya msingi au mtaalamu ikiwa unahitaji huduma zaidi.

Huduma za muda mrefu

ORR inatoa mipango ya ziada ambayo inaweza kukusaidia baada ya mwaka wako wa kwanza kuwa hapa. Mipango hii inalenga kukusaidia kuwa na usalama zaidi katika maisha yako nchini Marekani. Huduma hizi zinapatikana kwa muda wa hadi miaka 5.

Huduma za muda mrefu zinajumuisha:

Huduma za Msaada kwa Wakimbizi

Unaweza kupata huduma za msaada kwa hadi miaka 5 baada ya kuwasili Marekani. Huduma hizi zinajumuisha msaada wa kujifunza Kiingereza, kupata kazi, na mafunzo. Unaweza pia kupata msaada na huduma za malezi ya watoto, usafiri, tafsiri na ukalimani, na usimamizi wa kesi. Unaweza pia kupata elimu ya afya na msaada wa afya ya akili kupitia mpango huu.

Mipango maalum

Baadhi ya mashirika ya makazi mapya na mashirika ya kijamii hutoa mipango maalum kama vile akiba ya fedha, ushauri kwa vijana, huduma kwa wazee, na msaada wa kiufundi kwa biashara ndogo ndogo zinazoanzishwa.

Kuna nyenzo za ziada kwa makundi fulani. Pata maelezo zaidi kuhusu manufaa kwa waliopewa msamaha wa Ukreni na wanaowasiri kutoka Afghanstani.


Taarifa kwenye ukurasa huu inatoka USA.gov, Office of Refugee Resettlement, na vyanzo vingine vinavyoaminika. Tunakusudia kutoa taarifa rahisi kueleweka ambazo zinarekebishwa mara kwa mara. Taarifa hii sio ushauri wa kisheria.