Miongozo ya madereva iliyotafsiriwa kwa ajili ya wageni nchini Marekani
Pata miongozo ya madereva iliyotafsiriwa na taarifa ya jinsi ya kuendesha gari Marekani.
Mwongozo wa dereva ni nini?
Mwongozo wa dereva ni kitabu kidogo chenye taarifa ya jinsi ya kuendesha gari. Unafafanua sheria za udereva na kukuandaa kwa mitihani ya udereva. Ni kijitabu cha bure kutoka Idara ya Magari, inayojulikana pia kama DMV. Kila jimbo nchini Marekani lina mwongozo wake wa udereva.
Miongozo ya madereva Marekani iliyotafsiriwa
Miongozo hii ya madereva iliyotafsiriwa katika lugha yako ya kwanza itakusaidia kujiandaa kwa ajili ya mtihani wa udereva. Katika majimbo mengi, unaweza kufanya mitihani hii katika lugha yako. Katika majimbo mengine, lazima ufanye mtihani huu kwa Kiingereza.
MUHIMU: Miongozo hii si mahsusi kwa jimbo lako tu na huenda ikawa imepitwa na wakati. Itakusaidia wakati wa kujifunza lakini inapaswa kutumiwa kukusaidia tu kwani baadhi ya sheria zinaweza kuwa tofauti katika jimbo lako. Utahitaji pia mwongozo rasmi wa dereva kwa jimbo lako.
Bofya kwenye moja ya picha hapa chini ili kuona mwongozo wa dereva. Unaweza kusoma mwongozo mtandaoni, au kuupakua kwenye kompyuta au simu yako.
دليل السائق (Arabic)
Վարորդի ձեռնարկ (Armenian)
驾驶员手册 (Chinese)
کتاب رهنما دریوری (Dari)
دفترچه راهنمای راننده (Farsi)
Manuel du conducteur (French)
हिन्दी (Hindi)
運転マニュアル (Japanese)
ပှၤနီၣ်သိလ့ၣ် အလံာ်နဲၣ်ကျဲ (Karen)
សៀវភៅណែនាំស្ដីពីការបើកបរ (Khmer)
Igitabo cy’umushoferi (Kinyarwanda)
운전자 설명서 (Korean)
चालकलाई मार्गनिर्देशिका (Nepali)
د موټر چلوونکي لاسي کتاب (Pashto)
ਪੰਜਾਬੀ (Punjabi)
Руководство для водителя (Russian)
Buuga darawalnimada (Somali)
Manual del conductor (Spanish)
Mwongozo wa Dereva (Swahili)
ПІДРУЧНИК ВОДІЯ (Ukrainian)
số tay lái xe (Vietnamese)
Taarifa kwenye ukurasa huu umetoka kwa Department of Motor Vehicles (DMV), ReEstablish Richmond, na vyanzo vingine vinavyoaminika. Malengo yetu ni kutoa taarifa zilizo rahisi kuelewa na zinazosasishwa mara kwa mara. Taarifa hii si ushauri wa kisheria.