Miongozo ya udereva iliyotafsiriwa kwa wageni nchini Marekani

Imerekebishwa Mei 22, 2025
Pata miongozo na taarifa za udereva zilizotafsiriwa za jinsi ya kuendesha gari nchini Marekani.

Mwongozo wa dereva ni nini?

Mwongozo wa udereva ni kitabu kidogo ambacho kina taarifa kuhusu jinsi ya kuendesha gari. Kinaelezea sheria za udereva na kukuandaa kwa ajili ya mitihani udereva. Ni kitabu cha bila malipo kutoka Department of Motor Vehicles, pia hujulikana kama DMV. Kila jimbo nchini Marekani lina mwongozo wake wa udereva.

Miongozo ya udereva wa Marekani iliyotafsiriwa

Majimbo mengi yana miongozo ya udereva katika lugha tofauti ili kukusaidia kuelewa sheria za barabarani. Miongozo hii ya udereva iliyotafsiriwa katika lugha yako ya kwanza itakusaidia kujiandaa kwa ajili ya mtihani wa udereva. Baadhi ya majimbo yanakuruhusu kufanya mtihani wa maarifa ulioandikwa kwa lugha yako na kutumia mtafsiri wakati wa mtihani wa ujuzi wa barabarani.

Baadhi ya miongozo hii inaweza isiwe mahususi kwa jimbo lako na inaweza kupitwa na wakati. Tembelea tovuti ya Idara ya Vyombo vya Moto (DMV) ya jimbo lako kwa mwongozo wa hivi punde. Unaweza pia kuchukua nakala katika ofisi yako ya karibu ya Idara ya Vyombo vya Moto (DMV).

Bofya moja ya picha za hapa chini ili uone mwongozo wa udereva. Unaweza kuusoma mwongozo huo mtandaoni, au unaweza kuupakua kwenye kompyuta au simu yako ya mkononi.

دليل السائق (Kiarabu)

Mwongozo wa dereva wa kiarabu

 የአሽከርካሪዎች መመሪያ (Amharic)

Վարորդի ձեռնարկ (Kiarmenia)

Mwongozo wa dereva wa Kiarmenia

ယာဉ်မောင်းလမ်းညွှန် (Burmese)

Mwongozo wa dereva wa Kiburma

驾驶员手册 (Kichina)

Mwongozo wa dereva wa Kichina

کتاب رهنما دریوری (Kidari)

دفترچه راهنمای راننده (Kifarsi)

Manuel du conducteur (Kifaransa)

Manyèl ofisyèl lisans chofè (Krioli ya Haiti)

हिन्दी (Kihindi)

運転マニュアル (Kijapani)

Igitabo cy'umushoferi (Kinyarwanda)

운전자 설명서 (Kikorea)

चालकलाई मार्गनिर्देशिका (Kinepali)

د موټر چلوونکي لاسي کتاب (Kipashto)

mwongozo wa dereva wa California kwa Kipashto

Mwongozo wa dereva (Kireno)

ਪੰਜਾਬੀ (Kipunjabi),

Руководство для водителя (Kirusi)

Buuga darawalnimada (Kisomali)

Manual del conductor (Kispaniola)

Mwongozo wa dereva (Kiswahili)

jalada la mwongozo wa udereva kwa Kiswahili

Drayber manwal (Tagalog)

ПІДРУЧНИК ВОДІЯ (Kiukreni)

ڈرائیور کا دستی (Urdu)

Số tay lái xe (Vietnamese)


Taarifa kwenye ukurasa huu inatoka Department of Motor Vehicles (DMV), ReEstablish Richmond, na vyanzo vingine vinavyoaminika. Tunakusudia kutoa taarifa rahisi kueleweka ambazo zinarekebishwa mara kwa mara. Taarifa hii sio ushauri wa kisheria.