Mwongozo wa dereva ni nini?
Mwongozo wa udereva ni kitabu kidogo ambacho kina taarifa kuhusu jinsi ya kuendesha gari. Kinaelezea sheria za udereva na kukuandaa kwa ajili ya mitihani udereva. Ni kitabu cha bila malipo kutoka Department of Motor Vehicles, pia hujulikana kama DMV. Kila jimbo nchini Marekani lina mwongozo wake wa udereva.
Miongozo ya udereva wa Marekani iliyotafsiriwa
Miongozo hii ya udereva iliyotafsiriwa katika lugha yako ya kwanza itakusaidia kujiandaa kwa ajili ya mtihani wa udereva. Katika majimbo mengi, unaweza kufanya mitihani kwa lugha yako. Katika majimbo mengine, lazima ufanye mtihani kwa Kiingereza.
MUHIMU: Miongozo hii inaweza isiwe mahususi kwa jimbo lako na inaweza kupitwa na wakati. Inaweza kukusaidia kujifunza lakini inapaswa kutumika tu kukusaidia kwani baadhi ya sheria zinaweza kuwa tofauti katika jimbo lako. Unapaswa kuwa na mwongozo rasmi wa udereva wa jimbo lako pia.
Bofya moja ya picha za hapa chini ili uone mwongozo wa udereva. Unaweza kuusoma mwongozo huo mtandaoni, au unaweza kuupakua kwenye kompyuta au simu yako ya mkononi.
دليل السائق (Kiarabu)

Վարորդի ձեռնարկ (Kiarmenia)

驾驶员手册 (Kichina)

کتاب رهنما دریوری (Kidari)

دفترچه راهنمای راننده (Kifarsi)

Manuel du conducteur (Kifaransa)

Manyèl Ofisyèl Lisans Chofè (Kleole ya Haiti)

हिन्दी (Kihindi)

運転マニュアル (Kijapani)

ပှၤနီၣ်သိလ့ၣ် အလံာ်နဲၣ်ကျဲ (Kikareni)

សៀវភៅណែនាំស្ដីពីការបើកបរ (Kikhmeri)

Igitabo cy'umushoferi (Kinyarwanda)

운전자 설명서 (Kikorea)

चालकलाई मार्गनिर्देशिका (Kinepali)

د موټر چلوونکي لاسي کتاب (Kipashto)

ਪੰਜਾਬੀ (Kipunjabi),

Руководство для водителя (Kirusi)

Buuga darawalnimada (Kisomali)

Manual del conductor (Kispaniola)

Mwongozo wa Dereva (Kiswahili)

Drayber Manwal (Kitagalogi)

ПІДРУЧНИК ВОДІЯ (Kiukreni)

số tay lái xe (Kivietinamu)

Taarifa kwenye ukurasa huu inatoka Department of Motor Vehicles (DMV), ReEstablish Richmond, na vyanzo vingine vinavyoaminika. Tunakusudia kutoa taarifa rahisi kueleweka ambazo zinarekebishwa mara kwa mara. Taarifa hii sio ushauri wa kisheria.