Orodha kamili ya madarasa ya Kiingereza bila malipo mtandaoni na nyenzo nyingine muhimu
Kuna njia nyingi za kujifunza na kuboresha Kiingereza chako bila malipo kupitia kompyuta au simu yako. Pata orodha kamili ya madarasa ya Kiingereza bila malipo mtandaoni. Fahamu nini wanachofundisha na wapi kwenda ili kuanza.
Kujifunza Kiingereza mtandaoni
Orodha hii inatoa aina mbalimbali za madarasa ya Kiingereza, programu-tumizi na tovuti ili kukusaidia kujifunza Kiingereza kama lugha ya pili. Kila mtu anajifunza tofauti. Jaribu kila mojawapo nini kinachofaa zaidi kwako.
Madarasa ya Kiingereza bila malipo mtandaoni
Darasa | Kinachofundishwa | Tovuti/programu-tumizi | Usaidizi wa lugha ya 1 |
---|---|---|---|
Madarasa na video fupi za kujifunza maneno na misemo ya Kiingereza ili kusaidia katika maisha ya kila siku | Tovuti na programu-tumizi | Kiamhari, Kiburma, Kichina, Kidari, Kikorea, Kiajemi, Kithai | |
Madarasa shirikishi yenye masomo mafupi na mazoezi. Unaweza kufanyia mazoezi matamshi yako ya Kiingereza na wazungumzaji asilia. Huduma ya msingi haina malipo | Tovuti na programu-tumizi | ||
Tovuti ya lugha mbili kwa waelimishaji na familia za wanafunzi wa lugha ya Kiingereza | Tovuti | Kispaniola | |
Madarasa mbalimbali ya Kiingereza bila malipo kwa ngazi za mwanzo, kati na mwisho | Tovuti na programu-tumizi | Kiarabu, Kikatalani, Kifaransa, Kijerumani, Kiitaliano, Kireno, Kirusi, Kispaniola, Kivietinamu | |
Masomo mafupi, majaribio ya vitendo na marudio ili kukusaidia kujifunza Kiingereza | Tovuti na programu-tumizi | ||
Msaada kwa stadi za kusikiliza. Chagua mada kulingana na mambo yanayokuvutia kama vile michezo, historia au usafiri | Tovuti | ||
Michezo, video na nyimbo za kuwasaidia watoto kujifunza Kiingereza. Jisajili bila malipo kupitia USAHello | Programu-tumizi tu | ||
Shughuli za mtandaoni kwa kutumia video, picha, sauti, chati na maandishi. Hufundisha msamiati, sarufi, tahajia na stadi za maisha. Hukusaidia kufanya mazoezi ya kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika Kiingereza | Tovuti na programu-tumizi | Kispaniola | |
Masomo ya kila wiki ya video na karatasi zinazoweza kuchapishwa ili kujifunza Kiingereza. Kurasa za habari zenye orodha ya misamiati mipya na makala ili kupima ujuzi wako wa Kiingereza | Tovuti | Kiburma, Kikrioli, Kifaransa, Kihispania, Kiswahili, Kituruki, na nyingine nyingi |
Rasilimali za kujifunza Kiingereza bila malipo
Rasilimali | Kinachofundishwa | Aina |
---|---|---|
Shughuli za kujifunza, majaribio, michezo na rasilimali nyinginezo ili kuboresha matumizi ya Kiingereza cha maisha halisi | Tovuti | |
Jaribio la Kiingereza sanifu mtandaoni ili kupima kiwango chako cha Kiingereza. Cheti cha bure cha EF SET™ | Tovuti na programu-tumizi | |
Karatasi za kazi na maswali unayoweza kupakua ili kufanyia mazoezi Kiingereza chako | Tovuti | |
Rasilimali, ikiwemo mazoezi ya sarufi na msamiati | Tovuti | |
Fanya majaribio (kama vile TOEFL) ili kukusaidia kukutayarisha kwa majaribio ya lugha ya Kiingereza shuleni au mahali pa kazi. | Tovuti na programu-tumizi | |
Madarasa na rasilimali za Kiingereza, ikiwemo zaidi ya video 2000 za mazungumzo ya Kiingereza unazoweza kutazama ili kujifunza kuhusu utamaduni, historia na vitabu vya Marekani. | Tovuti | |
Inakagua maandishi yako na kusahihisha makosa yako ya sarufi | Tovuti na programu-tumizi | |
Majaribio ya kukusaidia kujifunza sarufi ya Kiingereza | Tovuti | |
Jifunze kuandika kwa Kiingereza kwa usaidizi kutoka kwa mzungumzaji asilia | Tovuti | |
Vidokezo vya sarufi na matamshi ili kuboresha uandishi wako na uakifishaji wa Kiingereza. Nyenzo za kuandika barua za kawaida za biashara, barua za kazi na wasifu | Tovuti |
Jifunze Kiingereza kwenye mitandao ya kijamii
Mitandao ya kijamii inatoa mamia ya nyenzo kwa wanaojifunza Kiingereza. Tiktok ina kila kitu, kama vile video kuhusu sarufi. YouTube ina video unazoweza kukariri na kujifunza kwa njia ya kufurahisha.
Je, kuna kitu kimekosekana kwenye orodha hii? Tujulishe. Tuma barua pepe kwa timu yetu kupitia [email protected]. Asante!
Malengo yetu ni kutoa taarifa zilizo rahisi kuelewa na zinazosasishwa mara kwa mara. Taarifa hii si ushauri wa kisheria.