Kuunganisha tena familia kwa wakimbizi na wahamiaji

Imerekebishwa Machi 14, 2025
Ukurasa huu ulitafsiriwa kitaalamu na mwanadamu. Jifunze zaidi

Wakimbizi, waomba hifadhi, na wamiliki wa SIV wa Afghan wanaweza kuomba baadhi ya wanafamilia kuunaga nao nchini Marekani. Pata maelezo zaidi kuhusu kuunganishwa tena kwa familia. Pata taarifa kuhusu mpango huu na jinsi ya kuomba.

Hali ya kuunganisha tena familia 

Uongozi mpya umekuwa ukifanya mabadiliko katika masuala ya uhamiaji jambo ambalo limeathiri kuunganisha tena familia, kama vile kusimamisha ushughulikiaji wa wakimbizi kupitia Mpango wa Uandikishaji wa Wakimbizi wa Marekani (USRAP). Pia, kwa sasa umezuia mashirika ya makazi mapya kutoa msaada kwa wakimbizi, waomba hifadhi, na SIV.

Wakimbizi na waomba hifadhi

  • Ombi la Ndugu wa Mkimbizi/Muomba Hifadhi la I-730 haliathiriwi. Bado unaweza kuomba, na kesi za kufuata kujiunga zinaendelea kushughulikiwa. Ushughulikiaji na uandikishaji wa wakimbizi ulisitishwa lakini sasa umeanza tena. Hata hivyo, bado kunaweza kuwa na ucheleweshaji au mabadiliko katika jinsi masuala hayo yanavyoshughulikiwa.

Wamiliki wa SIV wa Afghanistan na Iraki

  • Maombi ya Kufuata Kujiunga ya I-824 SIV hayaathiriwa. Bado unaweza kuomba, na masuala hayo yanaendelea kushughulikiwa. Msaada wa usafiri haupatikani tena. Lazima uandae usafari wako mwenyewe.

Parole ya Afghan

  • Kuunganisha Tena Familia ya Parole wa Afghan ya DS-4317 kumesitishwa. Bado unaweza kuwasilisha Fomu DS-4317, lakini mpango umesitishwa na huenda usianze tena.

Wairaki na Wasyria

  • Mpango wa Upatikanaji wa Moja kwa Moja wa P-2 umesitishwa. Huwezi kuomba au kuwaleta wanafamilia wako Marekani chini ya mpango maalum wa USRAP I-130. Bado unaweza kuomba uhamiaji wa familia kupitia mchakato wa kawaida wa I-130.

Wazazi wa watoto wadogo wa Amerika ya Kati

  • Mpango wa Watoto wa Amerika ya Kati (CAM) umesitishwa. Huwezi kuomba au kuleta familia yako kupitia CAM, masuala yote kwa sasa yamesimamishwa.

Mpango wa Hati ya Kiapo cha Uhusiano P-3

  • Mpango wa P-3 umesitishwa. Wakimbizi, waomba hifadhi, na wamiliki wa SIV nchini Marekani kwa sasa hawawezi kuomba kuunganisha familia kupitia AOR.

Mpango wa wakimbizi na waomba hifadhi

Kuna mipango maalum nchini Marekani kuwasaidia wakimbizi na waomba hifadhi kuungana tena na wanafamilia wao. Hizi ni pamoja na Fomu I-730 na Taarifa ya Uhusiano (AOR) kwa wakimbizi, wasili, na SIV na familia katika nchi za kipaumbele.

Programu hii hutoa faida kadhaa muhimu ikiwa ni pamoja na:

  • Hakuna ada ya maombi
  • Mwanafamilia wako atapokea hali sawa ya kisheria kama ulivyokuja nayo (hii inaitwa hali ya kuiga)
  • Unaweza kuwasilisha mara tu unapofika kama mkimbizi au mara tu unapopewa hifadhi (huna haja ya kusubiri hadi upate Green Card yako)
  • Wakati mwingine inaweza kuwa haraka kuliko michakato mingine

Ni muhimu kutuma maombi ya mipango hii haraka iwezekanavyo. Ukichelewa tarehe ya mwisho ya kuwasilisha, bado utaweza kuomba kuunganishwa na familia kupitia mchakato wa I-130 kama mmiliki wa Green Card au raia wa Marekani lakini hautapata faida inayolingana.

Fomu I-730 Maombi Yanayohusu Mkimbizi / Muomba Hifadhi

Fomu I-730 ni nini?

Kama wewe ulikuja Marekani kama mkimbizi au umepewa hifadhi, unaweza kutuma maombi kwa ajili ya ndugu yako ya karibu kwa kutumia Fomu I-730. Programu hii inakuwezesha kuomba kwa wanafamilia wako wa karibu pekee. Hii ni pamoja na:

  • Wenzi
  • Watoto ambao hawajaolewa wenye umri chini ya miaka 21

Wazazi, ndugu, binamu, shangazi, wajomba, na bibi/babu hawastahiki kwa mujibu wa mpango wa kuunganisha familia ya wakimbizi na watafuta hifadhi.

Kuwasilisha Fomu I-730 ndiyo njia kuu ya kumwombea mwanafamilia wako kuja Marekani. Lazima uombe ndani ya miaka 2 ya kuwasili Marekani kama mkimbizi au mwomba hifadhi.

Jinsi ya kuomba

Wakimbizi na waomba hifadhi wanaweza kuwasilisha Fomu I-730 kwa USCIS. Shirika lako la makazi mapya linaweza kukusaidia kupata mwakilishi wa kisheria ambaye anaweza kukusaidia kuhakikisha kuwa unajaza fomu kwa usahihi na linaweza kukusaidia kukusanya hati zinazohitajika.

  • Mwombaji mkuu: mtu anayetuma maombi akiomba mwanafamilia wake aje Marekani. Pia, wanajulikana kama mwombaji.
  • Mwombaji mnufaika: mwanafamilia ambaye mwombaji mkuu amewasilisha maombi kwa ajili yake. Pia, anajulikana kama mnufaika au wafuasi wa kujiunga na mkimbizi au muomba hifadhi.
Nani anaweza kuomba
Wakimbizi na Waomba Hifadhi
Makataa
Lazima utume maombi ndani ya miaka 2 ya kuingia Marekani kama mkimbizi au kupewa hadhi ya mtafuta hifadhi.
Wanafamilia
Mwenzi na watoto wasiooa/wasioolewa wenye umri chini ya miaka 21 (ulipopewa hadhi ya ukimbizi au mtafuta hifadhi)
Fomu
Wasilisha Fomu I-730 pamoja nyaraka za uthibitisho ikiwemo uthibitisho wa hadhi, uhusiano wa familia, na picha za wanafamilia
Fees
Hakuna ada
Muda wa uchakataji
Hivi sasa, USCIS inatumia wastani wa zaidi ya miezi 11 kushugulikia I-730. Kila suala ni tofauti na linaweza kutumia muda mwingi au kidogo zaidi kukamilika. Unaweza kufuatilia hali ya maombi yako mtandaoni.
Usaili
Ikiwa USCIS inaona kwamba ndugu yako anastahiki, watapanga usaili na mwanafamilia wako.
  • Ikiwa mwanafamilia wako yuko ndani ya Marekani, atahojiwa katika ofisi ya USCIS ya eneo lako.
  • Ikiwa wako nje ya Marekani, itakuwa katika ofisi ya kimataifa ya USCIS, ubalozi, au ubalozi mdogo wa Marekani.
  • Afisa atapitia maombi ya mwanafamilia wako na kufanya uamuzi kama wana sifa za kusafiri kuja Marekani.

    Kusafiri kwenda Marekani
    Akiidhinishwa, anapaswa kujaza makaratasi zaidi na hatua zinazohitajika kabla ya kusafiri. Atalazimika kufanya mipango yake mwenyewe ya kusafiri.

    Hati ya kiapo cha uhusiano (AOR)

    AOR ni hati ya kisheria ambayo inathibitisha uhusiano wa familia yako pamoja na ndugu zako wa nje ya nchi. Ukiwasilisha AOR huunganisha suala lako pamoja na suala la mwanafamilia wako. Jambo hili linaweza kuwasaidia wanafamilia wako kupata makazi mapya katika eneo lako.

    Wakimbizi, waomba hifadhi, na wamiliki wa SIV nchini Marekani kwa sasa hawawezi kuomba kuunganisha familia kupitia AOR. Hapo awali, AOR ingeweza kuwasilishwa kwa ajili ya wazazi wako, mwenzi wako, na watoto ambao hawajaoa/hawajaolewa wenye umri chini ya miaka 21 ambao wana hadhi ya ukimbizi.

    Mpango wa familia za Afghanistan

    Waafghanistani wana machaguo tofauti ya kuungana tena na wanafamilia, kulingana na hadhi yao. Ikiwa una hadhi ya ukimbizi au muomba hifadhi, fuata maelekezo ya hapo juu. Kwa wakazi wa kudumu, wanaweza kupata taarifa hapa. Pia, kuna machaguo mahususi kwa hadhi zingine za kipekee kwa Waafghanistani, ikiwemo:

    • Ikiwa wewe ni Muafghani ambaye alibadilisha hadhi na kuwa Mhamiaji Maalum unapokuwa Marekani, mwenzi wako au watoto wanaweza kuongezwa kwenye kesi yako ya SIV. Lazima uwasilishe Fomu I-824. Ikiwa USCIS inakubali ombi lako, NVC itawasiliana na wewe na wanafamilia wako kuanza mchakato wa maombi ya SIV.
    • Kuunganisha Tena Familia ya Parole wa Afghan ya DS-4317 kumesitishwa. Bado unaweza kuwasilisha Fomu DS-4317, lakini mpango umesitishwa na huenda usianze tena.

    Ni muhimu kupata ushauri wa kisheria ili kuelewa machaguo yako. Shirika lako la makazi mapya linaweza kukupa msaada. Mashirika na wanasheria wanaweza pia kukusaidia. Fahamu jinsi ya kupata huduma za kisheria za bure au za gharama nafuu.

    mwanasheria anayekagua taarifa
    Epuka ulaghai wa uhamiaji

    Fahamu jinsi ya kujilinda mwenyewe dhidi ya wathibitisha na tovuti bandia. Jifunze nini cha kufanya unapokuwa mwathirika wa udanganyifu.

    Pata Maelezo Zaidi

    Taarifa kwenye ukurasa huu inatoka UNHCR, USCIS, CLINIC, na vyanzo vingine vinavyoaminika. Tunakusudia kutoa taarifa rahisi kueleweka ambazo zinarekebishwa mara kwa mara. Taarifa hii sio ushauri wa kisheria.