Gawanya

Jinsi ya kuomba hifadhi Marekani

Hifadhi ni aina ya ulinzi unaokuwezesha kukaa Marekani. Pata taarifa za hivi karibuni kuhusu kutafuta hifadhi Marekani. Fahamu kama unastahiki na jinsi ya kuomba. Elewa jinsi ya kujiandaa kwa mahojiano.

Imesasishwa Juni 18, 2024

Muhimu: Kumewekwa sera mpya ambazo zinafanya kutafuta hifadhi kwenye mpaka wa Marekani na Mexico kuwa vigumu zaidi. Fahamu zaidi.

Hifadhi ni nini?

Hifadhi ni aina ya ulinzi unaokuwezesha kukaa Marekani ikiwa umeteswa au unahofia kuteswa katika nchi yako ya asili kwa sababu ya mbari yako, dini yako, utaifa wako, ushiriki wako katika kikundi fulani cha kijamii, au maoni yako ya kisiasa.

Ukipewa hifadhi, unaweza:

  • Kukaa Marekani kihalali ukiwa na ulinzi dhidi ya kuwekwa kizuizini na kufukuzwa nchini
  • Kuomba hifadhi kwa mwenzi wako na watoto
  • Kustahiki kiotomatiki kibali cha kufanya kazi nchini Marekani
  • Kumba kadi ya ‘social security’, hati za kusafiria, Green Card na uraia
  • Kuwa na ustahiki wa kupata huduma za makazi mapya kwakipindi fulani cha muda, ikiwemo usaidizi wa kifedha na matibabu, masomo ya Kiingereza, ajira, na huduma za afya ya akili.

Mateso ni nini?

Mateso ni pale unapotendewa vibaya kwa sababu ya mbari yako, dini, utaifa, kikundi cha kijamii, au maoni yako ya kisiasa. Hii inaweza kujumuisha madhara, vitisho, kufuatiliwa au kutazamwa mara kwa mara, kukamatwa bila haki, kuteswa, au kunyimwa haki za kimsingi kama vile uhuru wa kuongea au kuabudu kwa dini yako. Imanaanisha kuhisi hupo usalama na maisha au uhuru wako upo hatarini ukikaa nchini mwako.

Matakwa ya hifadhi

Unaweza kutafuta hifadhi ikiwa tu:

  • Unaogopa mateso katika nchi yako
  • Tayari upo nchini Marekani
  • Uliwasili Marekani chini ya mwaka mmoja uliopita (si kwa watu wote)
  • Bado hujapata makazi mapya katika nchi nyingine
  • Hujafanya uhalifu wa aina fulani au unachukuliwa kuwa tishio kwa usalama au ulinzi wa Marekani
(https://www.youtube.com/watch?v=Z0-BRWZztS8&list=PL845KO58lhKOannRoW0b0K42byIhNQrJT)

Kuomba hifadhi

Unapaswa kuomba hifadhi ndani ya mwaka mmoja baada ya kuwasili Marekani isipokuwa kama unakidhi hali maalum. Hakuna gharama au ada ya maombi. Hatua utakazochukua ni tofauti kulingana na ikiwa unatafuta hifadhi ya uthibitisho, hifadhi ya utetezi, au ulikuwa na uchunguzi chanya wa hofu sadikifu.

Kuna njia 3 za kupata hifadhi nchini Marekani:

Hifadhi ya uthibitisho [affirmative asylum]
Mchakato wa uthibitisho ni kwa watu wasio katika taratibu za kufukuzwa au kuondolewa. Afisa hifadhi wa Huduma za Uraia na Uhamiaji Marekani (USCIS) ndiye hukagua na kuamua kesi za uthibitisho.

Mahojiano ya ustahiki wa hifadhi [asylum merit interview]
Hii ni kwa wenye kesi za kuondolewa kwa haraka na walipata ubainifu chanya katika uchunguzi wao wa hofu sadikifu. Afisa hifadhi wa USCIS ndiye hukagua na kuamua kesi hizi.

Hifadhi ya utetezi [defensive asylum]
Mchakato wa utetezi ni kwa watu walio katika taratibu za kufukuzwa au kuondolewa nchini mbele ya hakimu wa uhamiaji wa Ofisi Kuu ya Ukaguzi wa Uhamiaji (EOIR). Jaji ndiye hupitia na kuamua kesi za utetezi.

You must apply for asylum within one year of arriving in the USA unless you meet an exception. There is no cost or fee to apply. The steps you take will be different depending on if you are seeking affirmative asylum, defensive asylum, or had a positive credible fear screening.

Unaweza kuwekwa katika taratibu za kuondolewa ikiwa:

  • Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka ya Marekani (CBP) inadai kwamba uliingia Marekani bila hati sahihi
  • Idara ya Uhamiaji na Ushurutishaji wa Forodha Marekani (ICE) ilikukamata ndani ya Marekani kwa kutokuwa na hadhi halali ya kisheria
  • Hifadhi yako ya uthibitisho haikuidhinishwa

Mchakato wa kupata hifadhi ni mgumu sana. Ni muhimu kupitia chaguzi zako za usaidizi wa kisheria. Mashirika na wanasheria wengi hutoa huduma na usaidizi wa kisheria bila malipo au kwa gharama nafuu. Utakuwa na nafasi nzuri ya kupata hifadhi ukimtumia wakili wa uhamiaji au mwakilishi wa uhamiaji aliyeidhinishwa. Wanaweza kukusaidia kujaza ombi lako na kujiandaa na mahojiano au usikilizaji wa shauri.

Mchakato wa hifadhi ya uthibitisho

Unapaswa kuwa Marekani au katika lango la kuingia nchini ili kuomba hifadhi. Lango la kuingia nchini inaweza kuwa uwanja wa ndege, bandari, au mpakani. Ikiwa haupo katika taratibu za kuondolewa, unaweza kuomba hifadhi ya uthibitisho moja kwa moja kupitia Huduma za Uraia na Uhamiaji Marekani (USCIS).

Unahitaji kujaza na kuwasilisha Fomu I-589.

Mchakato wa uchunguzi wa hofu sadikifu

Iwapo utawekwa katika taratibu za kuondolewa haraka na tuseme unataka kuomba hifadhi, utapelekwa USCIS kwa ajili ya uchunguzi wa hofu sadikifu.

Afisa hifadhi wa USCIS atakufanyia mahojiano ili kubaini kama una hofu sadikifu ya kuteswa au mateso. Anaweza kukuhitaji kwa mahojiano ya pili yanayoitwa Mahojiano ya Ustahiki wa Hifadhi au kukupeleka kwa hakimu wa uhamiaji kwa ajili ya mchakato wa kuomba hifadhi ya utetezi.

Mahojiano ya ustahiki wa hifadhi

Ikiwa una Mahojiano ya Ustahiki wa Hifadhi, atazingatia kama unastahiki ulinzi chini ya Mkataba Dhidi ya Mateso (CAT). Akiamua ya kwamba una ustahiki, utapewa hifadhi. Rekodi ya maandishi ya uamuzi chanya wa hofu sadikifu itatumika kama ombi lako la kuomba hifadhi. Hutahitajika kuwasilisha Fomu I-589.

Mchakato wa kuomba hifadhi ya utetezi

Ikiwa upo katika kituo cha kuzuiliwa wahamiaji cha Marekani au taratibu za kuondolewa, unaweza kuomba hifadhi ya utetezi kwa hakimu wa uhamiaji. Ikiwa huna ombi la hifadhi tayari kwenye faili, unapaswa kujaza na kuwasilisha Fomu I-589.

Kesi yako itakuwa hifadhi ya utetezi ikiwa:

  • umewekwa katika taratibu za kuondolewa baada ya USCIS kukunyima hifadhi ya uthibitisho
  • ulipaswa kuondolewa kwa haraka, ulionekana kuwa na hofu sadikifu, na ulipewa Notisi ya Kutokea (badala ya Mahojiano ya Ustahiki wa Hifadhi)
  • umewekwa katika taratibu za kuondolewa na ICE au CBP kwa ukiukaji wa uhamiaji

Mchakato wa kupata hifadhi ni mgumu sana. Ni muhimu kupitia chaguzi zako za usaidizi wa kisheria.

Hatua zinazofuata baada ya kupewa hifadhi

  1. Pata usaidizi wa huduma za makazi mapya.
  2. Omba kadi ya ‘social security’.
  3. Pata leseni ya udereva au kitambulisho cha serikali.
  4. Tafuta kazi. Unaweza kufanya kazi bila kulazimika kuomba kibali cha kazi au EAD.
  5. Kusafiri nje ya Marekani Lazima kwanza uombe kibali cha kusafiri. Wasilisha Fomu I-131 kwa USCIS kabla ya safari yako. Hati ya kusafiri ni halali kwa mwaka mmoja.
  6. Omba mwenzi wako na watoto wasio na ndoa walio chini ya miaka 21 waje Marekani Fahamu zaidi kuhusu kuunganisha tena familia.
  7. Omba Green Card mwaka mmoja baada ya kupata hifadhi.
  8. Omba uraia miaka 4 baada ya kupokea ukazi halali wa kudumu (Green Card).
lawyer reviewing information
Epuka ulaghai wa uhamiaji

Elewa jinsi ya kujilinda dhidi ya wanasheria feki (notarios) na tovuti bandia. Fahamu nini cha kufanya ikiwa umekuwa mhanga wa ulaghai.


Taarifa kwenye ukurasa huu umetoka kwa DHS, USCIS, na vyanzo vingine vinavyoaminika. Malengo yetu ni kutoa taarifa zilizo rahisi kuelewa na zinazosasishwa mara kwa mara. Taarifa hii si ushauri wa kisheria.

Share