Vidokezo vya kuzuia utapeli wa uhamiaji na ulaghai wa kawaida

Imerekebishwa Mei 15, 2025
Ukurasa huu ulitafsiriwa kitaalamu na mwanadamu. Jifunze zaidi
Utapeli wa uhamiaji ni wa kawaida sana na huchukua aina nyingi, kutoka kwa huduma za kisheria bandia hadi maafisa wa serikali wanaojifanya. Lazima ujue jinsi ya kujilinda. Pata vidokezo kuhusu jinsi ya kutambua, kuepuka na kuripoti ulaghai.

Utapeli wa uhamiaji ni nini?

Ulaghai au ulaghai ni wakati mtu anadanganya ili kuiba taarifa zako za kibinafsi au pesa. Ni kinyume cha sheria lakini ni kawaida. Unaweza kukutana na utapeli wa uhamiaji unapotuma maombi ya huduma za uhamiaji. Taarifa za kibinafsi hutumiwa kuiba utambulisho wako na zinaweza kujumuisha:

  • jina na anwani yako
  • akaunti ya benki na namba ya kadi ya mkopo
  • namba ya hifadhi ya jamii
  • nambari za bima ya afya

Ikiwa mtu anauliza maelezo haya, kuwa mwangalifu. Mpe tu mtu unayemwamini maelezo haya. Usimpe taarifa hii mtu yeyote anayeuliza kupitia simu, barua pepe, maandishi au mitandao ya kijamii.

Kashfa za ada ya uhamiaji

Ulaghai unaoomba malipo ya ada za uhamiaji ni jambo la kawaida. Ada na maombi ya uhamiaji yanashughulikiwa kupitia Huduma za Uraia na Uhamiaji za Marekani (USCIS), U.S. Department of State (DOS) na Idara ya Haki (DOJ) Ofisi Kuu ya Mapitio ya Uhamiaji (EOIR).

USCIS itakubali tu malipo mtandaoni kupitia akaunti yako ya myUSCIS au kwa njia ya posta kupitia maeneo yao rasmi ya lockbox. Unapokamilisha maombi mtandaoni, utaelekezwa kulipa ada kwenye pay.gov.

USCIS kamwe haitaomba:

  • Malipo kupitia simu au barua pepe
  • Malipo kupitia huduma kama vile Western Union, MoneyGram, PayPal, Venmo, Cash App, Zelle, kadi za zawadi au cryptocurrency 
  • Kutuma pesa kwa mtu au kumlipa mtu binafsi
Fomu zote za USCIS na EOIR za uhamiaji ni bure kwenye USCIS.gov na justice.gov. Hakuna mtu anayepaswa kukutoza kwa fomu.

Kuwa makini unapotafuta msaada wa kisheria. Ni mawakili tu na wawakilishi walioidhinishwa na DOJ ndiyo wanaoruhusiwa kutoa ushauri wa kisheria. 

Notarios Publicos

Katika nchi nyingi za Amerika ya Kusini na Ulaya, notario publicos (notaries public) ni mawakili wenye leseni walioidhinishwa kutoa ushauri wa kisheria.

Nchini Marekani, wathibitishaji husimamia viapo na kushuhudia kusainiwa kwa nyaraka muhimu. Nchini Marekani wathibitishaji rasmi hawana mafunzo au hawajaidhinishwa kutoa huduma zozote za kisheria. Nchini Marekani wathibitishaji wanaojaribu kukulaghai wanaweza:

  • Hujifanya wanatoa huduma za kisheria
  • Wanasaidaia kuwasilisha maombi ya USCIS bila utaalam unaohitajika
  • Huhifadhi hati zako asili
  • Kukuomba utie sahihi kwenye fomu tupu zenye taarifa za uongo 
  • Kutoa ushauri wa uongo wa kisheria unaosababisha matatizo katika kesi yako ya uhamiaji

Kidokezo:

Tovuti za utapeli wa uhamiaji

Tovuti ya utapeli wa uhamiaji inaweza kujifanya kutoa maelekezo na msaada wa kuwasilisha maombi ya USCIS. Tovuti za utapeli wakati mwingine hujaribu kuonekana kama tovuti rasmi na zinaweza kutumia mtindo unaofana au muhuri rasmi. Wanaweza kuwa na makosa ya kipekee ya kuandika.

Vidokezo:

  • Hakikisha tovuti iko salama kwa kutumia anwani ya “https” na alama ya kufuli (🔒)
  • Tovuti rasmi za serikali zinaishia kwa .gov
  • Tumia tovuti rasmi: USCIS.gov, DHS.gov, justice.gov
  • Pakua fomu za bure za serikali kutoka kwenye tovuti rasmi
  • Usitumie tovuti zinazojaribu kuwa na anwani inayofanana kama USCIS-online.org
  • Boresha mifumo ya simu na kompyuta zako pindi matoleo mapya yametoka
  • Tumia nenosiri thabiti na uthibitishaji wa vipengele viwili

Barua pepe za utapeli wa uhamiaji

Barua pepe za ulaghai ni za kawaida sana. Barua pepe nyingi za ulaghai zina faili au viungo vinavyopakua programu hasidi kwenye kifaa chako unapobofya. Wanaweza kuuliza taarifa za kibinafsi, kama vile nambari za akaunti, au kuomba malipo.

Barua pepe zinazotiliwa shaka zinaweza kuwa na:

  • Makosa yasiyo ya kawaida, kama vile katika jina lako
  • Herufi za ajabu na fonti zinazobadilika
  • Viungo kwenda kwenye tovuti bandia za serikali

Vidokezo:

  • Usifungue barua pepe zinazotiliwa shaka
  • Kuwa mwangalifu unapofungua barua pepe kutoka kwa mtu usiyemfahamu
  • Barua pepe zote kutoka USCIS au serikali ya Marekani zitamalizika wakati wote kwa .gov
  • Usibonyeze viungo vyovyote
  • Google au charaza anwani ya tovuti badala ya kubofya viungo
  • Usifanye malipo kupitia barua pepe
  • Usijibu barua pepe zinazotiliwa shaka
  • Kuwa makini na barua pepe yoyote inayodai kuwa na uamuzi wa USCIS
  • Nenda kwa myUSCIS ili uangalie kuwa unapata taarifa sahihi (sasisho zote muhimu zitakuwepo)
[email  protected] ni barua pepe ya ulaghai. Usifungue barua pepe kutoka kwa anwani hii au bonyeza viungo vyake chochote.

Utapeli wa uhamiaji na maandishi

Watu wengi hupigiwa simu na kutumiwa jumbe za ulaghai. Mara nyingi walaghai hubadilisha kitambulisho cha mpiga simu ili kuendana na msimbo wa eneo lako ili uweze kupokea.

Mpiga simu ya utapeli anaweza:

  • kujifanya kuwa afisa wa uhamiaji
  • kuomba taarifa binafsi au malipo
  • kusema taarifa zako si sahihi au unadaiwa ada na kutishia kukuripoti

Vidokezo:

  • USCIS haiombi taarifa binafsi au malipo kwa njia ya simu
  • Wasiliana na USCIS au EOIR ikiwa huna uhakika kama simu ni halisi
  • Tafuta mawasiliano ya shirika kwenye tovuti rasmi
  • Kata simu zinazotiliwa shaka na usijaribu kuzipigia
  • Zuia simu na jumbe za maandishi zisizohitajika
  • Wasiliana na wakili wa uhamiaji au mwakilishi ikiwa una maswali

Walaghai wanaweza pia kuwasiliana nawe kwenye mitandao ya kijamii ili kukupa usaidizi kuhusu ombi la uhamiaji, kama vile msamaha wa kibinadamu. USCIS haitawasiliana nawe kupitia Facebook, Twitter, LinkedIn, WhatsApp, au majukwaa mengine ya mtandaoni.

Kashfa za kawaida za uhamiaji

Hii hapa orodha ya mamlaka mahususi ya ulaghai wa uhamiaji wanashiriki na umma. Soma maagizo ya maombi ili kujua mahali pa kuyatuma na ujue ikiwa umeidhinishwa.

Ulaghai wa utekelezaji wa uhamiaji 

Walaghai wanaweza kuiga maafisa wa ICE ili kukulenga. Wanaweza kukupigia simu, kukutumia barua pepe, au kukutumia ujumbe kwenye mitandao ya kijamii wakiuliza taarifa za kibinafsi au pesa ili kuepuka kufukuzwa. ICE na polisi wa eneo hilo hawapaswi kuwasiliana na watu binafsi ili kuwaonya kuhusu kufukuzwa. 

Iwapo mtu atakusimamisha akidai kuwa afisa wa uhamiaji, uliza kuona beji yake na ujue ni idara gani anafanyia kazi. Usisaini karatasi yoyote bila wakili. Kuwa tayari kwa uvamizi wa ICE. 

Ulaghai wa taarifa za kibinafsi za Afghan

Ulaghai wa taarifa za kibinafsi za Afghan inaweza kukuuliza ushiriki maelezo ya kibinafsi ili kukusaidia kupata mafao ya uhamiaji. USCIS kwa ujumla haitumi barua pepe kukujulisha kuwa umeidhinishwa kwa mafao ya uhamiaji.

Kuharakisha usindikaji wa ulaghai 

Kuharakisha uchakachuaji kunaweza kuahidi kupata visa, Green Card, au kibali cha kufanya kazi haraka ikiwa utalipa ada. Wanaita hii "kuruka mstari." Wanaweza pia kusema wana wawasiliani serikalini ili kuharakisha kesi yako. Hakuna mtu anayeweza kuharakisha huduma zaidi ya nyakati za kawaida za usindikaji wa uhamiaji.

Ulaghai wa barua pepe wa Fomu I-9 

Ulaghai wa barua pepe wa Fomu I-9 unaweza kuwauliza waajiri maelezo ya Fomu I-9, wakijifanya kuwa maafisa wa USCIS. Waajiri si lazima wawasilishe Fomu I-9 kwa USCIS.

Kashfa za msamaha wa kibinadamu

Kashfa za msamaha wa kibinadamu zinaweza kulenga wahamiaji na wafadhili ili kuwachukua faida. Walaghai wanaweza kuwasiliana nawe mtandaoni au kupitia mitandao ya kijamii na kujitolea kuwa mfadhili wako kwa malipo ya ada au maelezo ya kibinafsi kama vile nambari yako ya pasipoti au tarehe ya kuzaliwa.

Wafadhili wanawajibika kutoa msaada wa kifedha kwa wanufaika kwa muda wa hadi miaka 2. Wanufaika hawapaswi kulipa au kufanya kazi kwa mfadhili wao. Wadhamini na wanufaika hawapaswi kulipa ada ya kuwasilisha maombi.

Utapeli wa usafirishaji haramu wa binadamu

Kashfa za usafirishaji haramu wa binadamu zinaweza kutokana na ulaghai wa ajira unaohusisha ofa za kazi zinazotiliwa shaka zinazotumwa ng'ambo au kwa barua pepe. Usafirishaji haramu wa binadamu unajumuisha hali ambapo unalazimishwa kufanya kazi na ushindwe kuondoka kwa sababu ya vitisho, madeni, na hali ya uhamiaji. Usimlipe yeyote anayekuahidi kazi au cheti.

Tafuta vidokezo vya usalama ili kuepuka usafirishaji haramu wa binadamu.

Kashfa za wakimbizi

Ulaghai wa wakimbizi hukuambia kuwa wanastahiki ruzuku maalum ya serikali na kukuomba ulipe kwanza au ushiriki maelezo yako ya benki. Ulaghai huu unaomba pesa ili kukusaidia na hali yako ya uhamiaji. 

kashfa za TPS

kashfa za TPS mara nyingi hutoa taarifa za uongo kuhusu kujiandikisha tena kwa TPS. Ulaghai huu unaweza kukuuliza uwasilishe fomu na malipo ili usasishe TPS yako. Ni bure kufanya upya. Usilipe au utume fomu yoyote hadi USCIS isasishe maelezo rasmi ya TPS mtandaoni.

Kashfa za bahati nasibu ya visa 

Kashfa za bahati nasibu ya visa inaweza kusema umechaguliwa kwa mpango wa visa anuai (DV). Idara ya Jimbo haitakutumia barua pepe kuhusu kuchaguliwa kwa bahati nasibu ya visa. Bahati nasibu ya visa ni bure. Huna haja ya kulipa ada ili kutuma maombi.

Jinsi ya kuripoti utapeli wa uhamiaji

Kuripoti utapeli wa uhamiaji kunaweza kukusaidia. Inaweza pia kusaidia kuhakikisha kwamba wengine hawapati kitu sawa. Unaweza kuripoti ulaghai bila kujulikana na sio lazima utoe jina lako. Unaweza pia kuwasilisha ripoti kwa niaba ya mtu mwingine.

Hakikisha unakusanya taarifa maalum kuhusu ulaghai au utapeli:

  • Tarehe, muda, na mahali pa tukio
  • Majina na mawasiliano ya mtu au biashara inayohusika
  • Maelezo ya ukiukaji
Ripoti kwa
Aina ya utapeli
Utapeli wa mafao ya uhamiaji
Utapeli wa uhamiaji
Utapeli wa kesi inayoendelea mahakamani
Utapeli wa usafirishaji haramu wa binadamu
Barua pepe, tovuti, au akaunti za mitandao ya kijamii zinazotiliwa shaka zinazodai kuwa zinahusika na USCIS
Utapeli wa jumla
Pesa au mali iliyopotea
Ulaghai
Utapeli wa mtandaoni
Udanganyifu na unyanyasaji wa mwajiri

Zungumza na mwanafamilia au rafiki unayemwamini au shirika lako la karibu la wahamiaji ikiwa unahitaji usaidizi. Tafuta usaidizi zaidi ikiwa mtu anakutishia.

Kuwa makini na taarifa nyingine za uongo

Kuna taarifa nyingi za uongo zinazosambazwa, hasa kuhusu suala la uhamiaji. Jihadharini na taarifa za upotoshaji na zisizo kamili.

Upotoshaji mara nyingi huitwa habari za uwongo. Imekusudiwa kushawishi maoni yako. Taarifa isiyo kamili haikusudii kukupotosha lakini bado inakupa taarufa isiyo sahihi.

Vidokezo:

  • Jihadhari na mahali ambapo habari na taarifa zako zinatoka
  • Kuwa makini na taarifa unazopata kwenye mitandao ya kijamii
  • Angalia vyanzo halisi ndani ya makala au chapisho
  • Soma kuhusu mwandishi na shirika ili kuona kama ni wa kuaminika
  • Thibitisha taarifa katika chanzo kingine

Taarifa kwenye ukurasa huu inatoka FTC, USCIS, DOJ, USA.gov, na vyanzo vingine vinavyoaminika. Tunakusudia kutoa taarifa rahisi kueleweka ambazo zinarekebishwa mara kwa mara. Taarifa hii sio ushauri wa kisheria.