Vidokezo vya kuzuia utapeli wa uhamiaji
- English (Kiingereza),
- አማርኛ (Kiamhari),
- العربية (Kiarabu),
- မြန်မာစာ (Kiburma),
- 简体中文 (Kichina),
- 繁體中文 (Kichina (cha jadi)),
- فارسی/دری (Kiajemi),
- Français (Kifaransa),
- Kreyòl Ayisyen (Mhaiti),
- हिन्दी (Kihindi),
- नेपाली (Kinepali),
- پښتو (Kipashto),
- Português (Kireno),
- ਪੰਜਾਬੀ (Punjabi),
- Русский (Kirusi),
- Af Soomaali (Msomali),
- Español (Kihispania),
- українська (Kiukreni),
- Tiếng Việt (Kivietinamu)
Utapeli wa uhamiaji ni jambo lililoenea sana na upo wa aina nyingi. Unapaswa kujua jinsi ya kujilinda. Pata vidokezo kuhusu jinsi ya kutambua, kuepuka na kuripoti utapeli.
Utapeli ni nini?
Ultapeli au udanganyifu ni pale mtu anapodanganya ili kuiba taarifa zako binafsi au pesa. Ni kinyume cha sheria lakini upo kila mahali. Taarifa binafsi hutumiwa kuiba utambulisho wako na zinaweza kujumuisha:
- jina na anwani yako
- akaunti ya benki na nambari za kadi ya benki
- nambari ya ‘social security’
- nambari za bima ya matibabu
Ikiwa mtu anaulizia taarifa hizi, kuwa mwangalifu. Mpe tu mtu unayemwamini taarifa hizi.
Utapeli wa malipo
Utapeli wa kuomba malipo ya ada za uhamiaji ni jambo la kawaida. Ada na maombi ya uhamiaji yanashughulikiwa kupitia Huduma za Uraia na Uhamiaji za Marekani (USCIS), Idara ya Serikali ya Marekani (DOS), na Ofisi Kuu ya Ukaguzi wa Uhamiaji (EOIR).
USCIS inakubali malipo mtandaoni tu kupitia akaunti yako ya myUSCIS au kwa barua kupitia maeneo yao rasmi ya kisanduku cha kufuli. Unapojaza maombi mtandaoni, utaelekezwa kulipa ada kupitia pay.gov.
USCIS kamwe haitaomba:
- Malipo kwa njia ya simu au kwa barua pepe
- Malipo kupitia huduma kama vile Western Union, MoneyGram au PayPal
- Kutuma pesa kwa mtu fulani au kumlipa mtu binafsi
Fomu zote za USCIS na EOIR ni bure kwenye USCIS.gov na justice.gov . Hakuna mtu anayepaswa kukutoza kwa fomu. |
Utapeli wa masuala ya kisheria
Kuwa mwangalifu unapotafuta usaidizi wa kisheria. Mawakili na wawakilishi walioidhinishwa na DOJ tu ndiyo wameidhinishwa kutoa ushauri wa kisheria.
Notarios Publicos
Katika nchi nyingi za Amerika ya Kusini na Ulaya, ‘notario publicos’ (makamishna wa viapo) ni mawakili wenye leseni walioidhinishwa kutoa ushauri wa kisheria.
Nchini Marekani, ‘notario publicos’ husimamia masuala ya viapo na kushuhudia utiaji saini wa hati muhimu. Makamishna wa viapo nchini Marekani hawana mafunzo au hawajaidhinishwa kutoa huduma zozote za kisheria. Notarios wa nchini Marekani ambao wanajaribu kukutapeli wanaweza:
- Kujifanya wanatoa huduma za kisheria
- Kujitolea kuwasilisha maombi ya USCIS bila utaalamu unaohitajika
- Kutoa ushauri wa kisheria usio sahihi ambao husababisha matatizo katika suala lako la uhamiaji
Kidokezo:
Hakikisha unapata ushauri wa kisheria kutoka kwa wakili wa uhamiaji mwenye leseni au mwakilishi wa kisheria aliyeidhinishwa. Fahamu jinsi ya kupata watoa huduma za kisheria unaoweza kuwaamini.
Tovuti za utapeli
Tovuti ya utapeli wa uhamiaji inaweza kujifanya inatoa maelekezo na kusaidia kuwasilisha maombi ya USCIS. Tovuti za utapeliwakati mwingine hujaribu kufanana na tovuti rasmi na zinaweza kutumia mtindo sawa au muhuri rasmi. Zinaweza kuwa na makosa ya uandishi yasiyo ya kawaida.
Vidokezo:
- Hakikisha kuwa tovuti ipo salama kwa kutumia anwani ya “https” na ikoni ya kufuli (🔒)
- Tovuti rasmi za serikali zinaishia kwa .gov
- Tumia tovuti rasmi: USCIS.gov, DHS.gov, justice.gov
- Pakua fomu za bila malipo za serikali kutoka tovuti rasmi
- Usitumie tovuti zinazojaribu kuwa na anwani sawa kama USCIS-online.org
- Sasisha simu yako na mifumo ya kompyuta pale matoleo mapya yanapotolewa
- Tumia nenosiri madhubuti na uthibitishaji wa vipengele vingi
Barua pepe za utapeli
Barua pepe za utapeli ni jambo lililoenea sana. Barua pepe nyingi za utapeli zina mafaili au viungo vinavyopakua programu hasidi kwenye kifaa chako unapovibofya. Zinaweza kuomba taarifa binafsi kama vile nambari za akaunti au kuomba malipo.
Barua pepe zenye mashaka zinaweza kuwa na:
- Makosa ya uandishi yasiyo ya kawaida, kama vile katika jina lako
- Vibabu vya ajabu na fonti tofauti
- Viungo vya tovuti ghushi za serikali
Vidokezo:
- Usifungue barua pepe zenye mashaka
- Kuwa mwangalifu unapofungua barua pepe kutoka kwa mtu usiyemjua
- Barua pepe zote kutoka USCIS au serikali ya Marekani zitaishia kwa .gov kila wakati
- Usibofye viungo vyovyote
- Google au andika anwani ya tovuti badala ya kubofya viungo
- Usifanye malipo kupitia barua pepe
- Usijibu barua pepe zenye mashaka
- Kuwa mwangalifu na barua pepe yoyote inayosema ina uamuzi wa USCIS
- Nenda myUSCIS ili kuangalia kuwa unapata taarifa sahihi (taarifa zote mpya na muhimu zitakuwepo)
[email protected] ni barua pepe ya utapeli. Usifungue barua pepe kutoka anwani hii au kubofya viungo vyake vyovyote. |
Simu na jumbe za utapeli
Watu wengi hupokea simu na jumbe za utapeli. Mara nyingi matapeli hubadilisha nambari ya simu ili iendane na msimbo wa eneo lako ili uweze kupokea. Aina zilizoenea zaidi ni kuhusu kadi za benki na kodi lakini baadhi zinaweza kuwa za uhamiaji.
Tapeli anayepiga simu anaweza:
- kujifanya afisa wa uhamiaji
- kuomba taarifa binafsi au malipo
- kusema taarifa zako si sahihi au unadaiwa ada na kutishia kukuripoti
Vidokezo:
- USCIS haiombi taarifa binafsi au malipo kupitia simu
- Wasiliana na USCIS au EOIR ikiwa huna uhakika kama simu ni ya kweli
- Tafuta anwani za wakala kwenye tovuti rasmi
- Kata simu zenye mashaka na usijaribu kuzipigia tena
- Zuia kupokea simu na jumbe zisizohitajika
- Wasiliana na wakili au mwakilishi wa masuala ya ikiwa una maswali
Matapeli wanaweza pia kuwasiliana nawe kwenye mitandao ya kijamii ili kukupa usaidizi wa kutuma maombi ya uhamiaji kama vile msamaha wa masuala ya kibinadamu. USCIS haitawasiliana nawe kupitia Facebook, Twitter, LinkedIn, WhatsApp, au majukwaa mengine ya mtandaoni.
Utapeli mwingine wa uhamiaji
Hii ni orodha ya utapeli wa uhamiaji ambao mamlaka zimeshirikisha kwa umma.
Ulaghai wa taarifa binafsi wa Afghanistan unaweza kukuomba ushiriki taarifa binafsi ili kukusaidia kupata mafao ya uhamiaji. USCIS kwa ujumla haitumi barua pepe kukujulisha kuwa umeidhinishwa kwa mafao fulani ya uhamiaji.
Utapeli wa kuharakisha mchakato unaweza kuahidi kupatia haraka visa, Green Card, au kibali cha kufanya kazi ikiwa utalipa ada. Hii inaitwa “kuruka foleni.” Wanaweza pia kusema wana watu wao serikalini wanaoweza kuharakisha jambo lako. Hakuna mtu anayeweza kuharakisha huduma zaidi ya muda wa kawaida wa ushughulikiaji.
Utapeli wa barua pepe ya Fomu I-9 unaweza kuwaomba waajiri taarifa za Fomu I-9 kwa kujifanya ni maafisa wa USCIS. Waajiri si lazima wawasilishe Fomu I-9 kwa USCIS.
Utapeli wa msamaha wa masuala ya kibinadamu unaweza kulenga wahamiaji na wafadhili kuwatapeli. Matapeli wanaweza kuwasiliana nawe mtandaoni au kupitia mitandao ya kijamii na kujitolea kuwa msaidizi wako kwa malipo ya ada au taarifa binafsi kama vile nambari yako ya pasipoti au tarehe ya kuzaliwa. Ikiwa unatafuta mfadhili, tumia Welcome Connect.
Wafadhili wana jukumu la kutoa usaidizi wa kifedha kwa walengwa kwa hadi miaka 2. Wanufaika hawalazimiki kumlipa au kumtumikia mfadhili wao. Wafadhili na wanufaika si lazima walipe ada ili kutuma maombi.
Utapeli wa biashara haramu ya binadamu unaweza kutokana na utapeli wa ajira ambao unahusisha ofa za kazi zinazotia mashaka zinazotumwa ng’ambo au kwa barua pepe. Biashara haramu ya binadamu unajumuisha hali ambapo watu wanalazimishwa kufanya kazi na hawawezi kuondoka kwa sababu ya vitisho, madeni, na hali ya uhamiaji. Pata vidokezo vya usalama ili kuepuka biashara haramu ya binadamu.
Utapeli wa TPS mara nyingi hutoa taarifa za uongo kuhusu kujisajili upya kwa TPS. Utapeli huu unaweza kukuomba uwasilishe fomu na malipo ili ufufue TPS yako. Ni bure kufufua. Usilipe au kuwasilisha fomu yoyote hadi USCIS isasishe taarifa rasmi ya TPS mtandaoni.
Utapeli wa bahati nasibu ya Visa unaweza kusema umechaguliwa kwenye programu ya Diversity Visa (DV). Bahati nasibu ya visa inasimamiwa na Idara ya Serikali, si USCIS. Idara ya Serikali haitakutumia barua pepe kuhusu kuchaguliwa kwenye bahati nasibu ya visa. Bahati nasibu ya visa ni bure. Huhitaji kulipa ada ili kutuma maombi.
Ripoti udanganyifu na utapeli
Kuripoti utapeli kunaweza kukusaidia. Inaweza pia kusaidia kuhakikisha kwamba wengine hawapati kitu kama hicho. Unaweza kuripoti utapeli bila kujulikana na sio lazima utoe jina lako. Unaweza pia kuwasilisha ripoti kwa niaba ya mtu mwingine.
Hakikisha umekusanya taarifa mahsusi kuhusu udanganyifu au utapeli huo:
- Tarehe, saa na eneo la tukio
- Majina na taarifa za mawasiliano ya mtu binafsi au biashara inayohusika
- Maelezo kuhusu ukiukaji
Ripoti kwa | Aina ya utapeli |
---|---|
Utapeli wa mafao ya uhamiaji | |
Utapeli wa uhamiaji | |
Utapeli wa mashauri ya mahakama ya uhamiaji | |
Utapeli wa biashara haramu ya binadamu | |
Barua pepe, tovuti au akaunti za mitandao ya kijamii inayotia mashaka ambazo zinadai kuwa na uhusiano na USCIS | |
Utapeli wa jumla | |
Pesa au mali iliyopotea | |
Udanganyifu | |
Utapeli wa mtandao | |
Udanganyifu na unyanyasaji wa mwajiri |
Zungumza na mwanafamilia au rafiki unayemwamini ikiwa unahitaji usaidizi. Tafuta usaidizi zaidi ikiwa mtu anakutishia.
Kuwa makini na taarifa nyingine za uongo
Kuna habari nyingi za uwongo zinazoshirikiwa, haswa karibu na mada ya uhamiaji. Jihadharini na taarifa zisizo sahihi. Taarifa potofu mara nyingi huitwa habari za uwongo. Imekusudiwa kushawishi maoni yako. Taarifa potofu hazikusudii kukupotosha kimakusudi lakini bado hukupa taarifa zisizo sahihi.
Vidokezo:
- Zingatia mahali habari na taarifa zako zinapotoka
- Kuwa mwangalifu na taarifa unazopata kwenye mitandao ya kijamii
- Kagua vyanzo vya asili ndani ya makala au chapisho
- Soma kuhusu mwandishi na shirika ili kuona kama wanaaminika
- Thibitisha habari katika chanzo kingine
Taarifa kwenye ukurasa huu umetoka kwa USCIS, FTC, DOJ, USA.gov, na vyanzo vingine vinavyoaminika. Malengo yetu ni kutoa taarifa zilizo rahisi kuelewa na zinazosasishwa mara kwa mara. Taarifa hii si ushauri wa kisheria.