Gawanya

Pata usaidizi wa utafsiri bila malipo nchini Marekani

Je, unahitaji usaidizi kuhusu tafsiri au ukalimani wa Kiingereza? Pata maelezo kuhusu haki zako za usaidizi wa utafsiri bila malipo na jinsi ya kuuomba. Tafuta njia za kupata tafsiri bila malipo katika lugha yako.

Imesasishwa Januari 26, 2024

Mkalimani na mfasiri ni nini?

Wakalimani na wafasiri huwasilisha ujumbe kutoka lugha moja hadi nyingine. Wanasaidia watu kuzungumza na kuelewa maandishi katika lugha tofauti.

Wakalimani hutafsiri maneno yaliyosemwa na yaliyoonyeshwa kwa ishara. Wakalimani wanaweza kufanya kazi ana kwa ana, kupitia simu au video.

Wafasirihufasiri maandishi yaliyoandikwa. Hii inajumuisha maandishi katika hati, vitabu na video.

Haki yako ya kuwa na mkalimani na mfasiri

Una haki ya kupokea usaidizi bila malipo wa utafsiri na ukalimani katika lugha yako kutoka kwa mashirika mengi ya serikali ya Marekani. Hii ni bila malipo kwa watu walio na uelewa mdogo wa Kiingereza (LEP), na inaitwa Ufikiaji wa Lugha.

Ikiwa huzungumzi Kiingereza kwa ufasaha, omba usaidizi. Ofisi hizi haziwezi kukataa kukupa huduma kwa sababu ya lugha yako.

Vidokezo vya kuomba usaidizi wa lugha:

 • Tumia programu kama Tarjimly au Google Translate ili kuwasiliana mahitaji yako.
 • Uliza kama kuna hatua fulani za kufuata ili kuomba mkalimani au tafsiri. Baadhi wanaweza kukuomba utume ombi mtandaoni. Pia, ofisi kawaida huhitaji kupanga mkalimani kabla ya miadi yako.
 • Shiriki lugha au lahaja unayopendelea. Kwa mfano, sema “I speak Swahili. I need an interpeter.”
 • Shiriki mapendeleo mengine , kama vile kuwa na mkalimani wa kike au wa kiume. 
 • Shiriki ikiwa utaleta mkalimani wako mwenyewe . Wanaweza kuwa na sheria kuhusu nani anayeweza kukutafsiria.
Unaweza pia kuomba usaidizi wa lugha ikiwa wewe ni kiziwi, mgumu wa kusikia, au una ulemavu wa kuzungumza. Piga 711 kwa usaidizi bila malipo wa kuwasiliana kupitia simu katika majimbo na wilaya zote 50.

 

Huduma za mkalimani katika ofisi za serikali:

Ripoti tatizo. Ikiwa hutapata huduma ya lugha unayopaswa, unaweza kuwasilisha malalamiko. Uliza mahali palipopaswa kukusaidia jinsi ya kufanya hivi. Wana hatua za kuangalia kile kilichotokea. Unaweza pia kuwasilisha malalamiko kwa Idara ya Haki ya Marekani.

Kupata mkalimani au mfasiri wako mwenyewe

Baadhi ya maeneo ambayo si sehemu ya serikali yanaweza kukosa kutoa usaidizi wa kutafsiri. Ikiwa unahitaji kupata msaada mwenyewe, unaweza:

 • Wasiliana na mwanafamilia au rafiki unayemwamini kwa usaidizi.
 • Uliza shirika lako la makazi mapya la wakimbizi kwa usaidizi wa bila malipo.
 • Tumia programu zisizolipishwa kwenye simu yako kama vile Tarjimly na Google Transalte.
 • Pata usaidizi bila malipo kupitia mashirika kama vile Tafsiri ya Kushughulikia Mgogoro.
 • Ajiri mfasiri au mkalimani wa kujitegemea.

Programu ya Tarjimly

Tarjimly inatoa usaidizi wa utafsiri bila malipo kwa wakimbizi, wanaotafuta hifadhi, na wafanyakazi wa misaada katika zaidi ya lugha 121. Katika programu ya Tarjimly, unaweza kuungana na mtafsiri aliyejitolea na kuanzisha mazungumzo. Unaweza kutuma ujumbe, ujumbe wa sauti, picha, au kupiga simu.

(https://youtu.be/JHG17Y5vR6M?si=Jt2xLZdV1DwBypSA)

Google Translate

Google Translate ni zana ya kutafsiri lugha ya mashine. Inatafsiri maandishi na hotuba katika zaidi ya lugha 100 katika kivinjari chako au kutoka kwa programu ya simu.

Ukiwa na Google Translate unaweza:

 • Kuzungumza kwenye programu na itajibu.
 • Kutafsiri mazungumzo katika muda halisi.
 • Kuandika kwa mkono au kuchapa maandishi.
 • Kutumia kamera yako kutafsiri maandishi.
 • Kutafsiri ukurasa mzima wa wavuti.
(https://www.youtube.com/watch?v=XaBrwzPQbhM)
Google Translate mara nyingi si sahihi 100%. Ubora wa tafsiri unaweza kutofautiana, kulingana na lugha iliyotafsiriwa.

Huduma nyingine za utafsiri bila malipo

Tafsiri ya Kushughulikia Mgogoro inatoa usaidizi wa utafsiri na ukalimani katika lugha 105.
Mradi wa Tafsiri ya Wakimbizi unatoa usaidizi wa tafsiri kwa wakimbizi na wanaotafuta hifadhi katika lugha 16.

Jinsi tafsiri na ukalimani unavyofanya kazi

Watafsiri na wakalimani wa kitaalamu wanapaswa kufuata sheria fulani.

Urefu
 Tafsiri na ukalimani wa kitaalamu si neno kwa neno. Inaweza kutumia maneno mengi au machache na kuchukuwa muda kutafsiri lugha yako hadi Kiingereza na kinyume chake.

Mtindo
 Wakalimani wanaweza kufanya kazi kwa njia mbili. Wanaweza kutafsiri kile kinachosemwa mara moja (wakati huo huo), au wanaweza kusubiri na kutafsiri baada ya sentensi chache (mfululizo).

Usahihi
 Wakalimani na wafasiri lazima wawasiliane hasa kile kinachozungumzwa au kuandikwa bila kubadilisha maana. Hawawezi kuongeza au kufuta maelezo ili kuhakikisha tafsiri sahihi.

Wakalimani wanaweza kukuuliza ufafanue neno au kifungu fulani cha maneno ili kuhakikisha kuwa wanakuelewa.

Usiri
 Kwa mujibu wa sheria, wakalimani wa kitaalamu na wafasiri lazima waweke siri taarifa zako zote. Hawawezi kushiriki maelezo yako na mtu yeyote bila idhini yako.

Vidokezo vya kuwasiliana na mkalimani

 • Zungumza na mtoa huduma, si mkalimani.
 • Ongea kwa uwazi na polepole, ukitumia kauli fupi zenye sentensi 1-2 kwa wakati mmoja.
 • Subiri mkalimani amalize kabla ya kuendelea.
 • Ikiwa huelewi kitu, mfahamishe. 
 • Mwombe arudie au aelezee maneno. 
FindHello app Houston search map
Find help near you

Find legal help, English classes, health clinics, housing support, and more. Search a local map and list of services for immigrants in the USA with the app FindHello.

Start your search

Taarifa kwenye ukurasa huu umetoka kwa our partner Tarjimly, USCIS, LawHelp.org, na vyanzo vingine vinavyoaminika. Malengo yetu ni kutoa taarifa zilizo rahisi kuelewa na zinazosasishwa mara kwa mara. Taarifa hii si ushauri wa kisheria.

Share