Gawanya

Msaada wa ukatili wa majumbani kwa wahamiaji

Ukatili wa majumbani si jambo la kupuuzwa. Inaweza kuwa vigumu hasa kwa wahamiaji ambao wanakabiliwa na changamoto zao za kipekee. Elewa ukatili wa majumbani ni nini. Fahamu haki zako ni zipi na jinsi ya kupata msaada.

Imesasishwa Oktoba 30, 2023

Kuondoka katika ukurasa huu, bofya kitufe chekundu cha kutoka. Mtu anayekunyanyasa anaweza kuangalia unachofanya kwenye intaneti, hakikisha unafuta historia ya kivinjari chako.

Je, unatafuta msaada kwa sasa? Ruka chini kupata taarifa ya msaada.

Ukatili wa majumbani ni nini?

Ukatili wa majumbani ni pale mtu katika familia au kaya yako anapojaribu kukudhibiti au kukudhuru. Hujulikana pia kama ukatili unaofanywa na mtu wa karibu au unyanyasaji wa majumbani.

Unaweza kutokea kwa mtu yeyote bila kujali umri, rangi, jinsia, mwelekeo wa kingono, au dini. Ingawa kesi nyingi zinazoripotiwa zinahusisha wanawake, wanaume nao pia ni wahanga. Mara nyingi ukatili wa majumbani unarejelea unyanyasaji kati ya watu wa karibu lakini unaweza kujumuisha:

 •  Mwenzi au mpenzi
 •  Mpenzi wa zamani
 • Mzazi mwenzako
 • Mwanafamilia, kama vile mzazi, mtoto, au ndugu
 • Mpangaji mwenzako au mtu unayeishi naye

Aina za unyanyasaji

Ishara za kawaida za ukatili wa majumbani ni:

 • Kudhuru mwili wako kama vile kukupiga ngumi, kukupiga mateke, kukusukuma, au kukurushia vitu. Hii inajulikana kama unyanyasaji wa kimwili.
 • Kukugusa bila ridhaa kama vile kukubusu au kukufanyia vitendo vya kingono bila ridhaa yako au kukulazimisha ufanye ngono. Katika ndoa hii inaweza kuchukuliwa ni unyanyasaji.
 • Kutoa lugha chafu na yenye kuumiza kama vile vitisho, kukutukana, kukufokea, kukuaibisha mbele ya watu wengine. Hii inajulikana kama unyanyasaji wa kihisia.
 • Kudhibiti pesa zako kama vile kuichukua, kukataa kukupa pesa za mahitaji muhimu, au kuzuia kutumia akaunti. 
 • Kukufanyia maamuzi, kukulazimisha kufanya mambo usiyotaka kufanya na njia nyingine za kukudhibiti.
 • Kukagua simu yako na jumbe za intaneti au kufuatilia mambo unayofanya, na kutaka kujua jinsi unavyotumia muda wako.
 • Kukuweka mbali na marafiki, familia na jumuiya kwa kukukataza kuonana au kuongea nao au kukutenga na jumuiya yako ya kitamaduni au kidini.
 • Kuja kwako bila taarifa, kukufuatilia, au kukutumia jumbe nyingi au kukupigia simu nyingi ambazo hukufanya uingiwe na hofu. Hii inajulikana kama kufuatilia-fuatilia.
 • Kuwatukana au kuwatishia wapendwa wako au kuharibu vitu vyako vya thamani na vitu uvipendavyo
 • Kutumia silaha ili kukuogopesha kama vile vitisho kwa kutumia kisu, bunduki, au gongo.
 • Kutokuruhusu ufanye kazi au uende shule.
 • Kuwa na wivu kupita kiasi kwako wewe na marafiki zako, au kukulaumu kuwa unafanya uzinzi.

Ukatili wa majumbani unajumuisha tabia tofauti tofauti na si lazima uwe wa kimwili kila wakati. Ishara hizi inawezekana zisijitokeze hadi uhusiano ukiwa umekomaa au hujitokeza kwa vipindi vipindi.

Manusura wengi wa ukatili wa majumbani hujilaumu wenyewe kwa unyanyasaji waliofanyiwa. Kumbuka, ukatili wa majumbani kamwe si kosa lako.

Wahamiaji na unyanyasaji

Wahamiaji wanaofanyiwa vitendo vya unyanyasaji wanapitia changamoto za kipekee kwa sababu ya hali yao ya uhamiaji. Unaweza kuhisi kutengwa na jumuiya yako na kwamba huna pa kupata msaada. Huenda hujui sheria na haki zinazohusiana na ukatili wa majumbani nchini Marekani.

Mnyanyasaji wako anaweza kutumia hali yako ya uhamiaji kukudhibiti au kukuzuia kupata msaada. Mnyanyasaji wako anaweza kutumia hofu yako ya kufukuzwa nchini ili kukufanya usiripoti vitendo vya unyanyasaji.

Mifano ya kawaida inaweza kuwa kwamba mnyanyasaji wako:

 • Ameshikilia hati/nyaraka zako za uhamiaji
 • Anakuzuia kupata hati/nyaraka za utambulisho
 • Anaharibu hati/nyaraka za kisheria kama leseni ya udereva na pasipoti.
 • Anakuzuia kutuma maombi ya uhamiaji
 • Hataki kutuma maombi ya uhamiaji kwa niaba yako
 • Anakutishia wewe au wapendwa wako mtafukuzwa nchini
 • Anakuzuia kujifunza Kiingereza

Kutafuta msaada wa uhamiaji

Nchini Marekani, kuna msaada kwa wahamiaji ambao ni wahanga wa ukatili wa majumbani. Unaweza kuwa na uwezo wa:

Ni muhimu kupata ushauri wa kisheria wakati unapofikiria chaguzi zako. Mwanasheria au mwakilishi aliyeidhinishwa anaweza kukusaidia kujua kama una ustahiki na kujaza maombi yako. Mashirika na wanasheria wengi hutoa msaada wa kisheria bila malipo au kwa gharama ndogo.

 Fahamu haki zako

Ni muhimu kujua haki zako na sheria za nchini Marekani. Ni haki yako kuwa salama na kupata usaidizi bila kujali hali yako ya uhamiaji.

Mtu yeyote anayefanyiwa vitendo vya unyanyasaji ana haki ya:

 • Kupata msaada kutoka vyombo vya sheria
 • Kumfungulia mashtaka ya jinai mnyanyasaji wake
 • Kupata hifadhi ya dharura
 • Kupata matibabu ya dharura
 • Kupata makazi ya muda mfupi
 • Kupata ushauri nasaha kwa tatizo lake
 • Kupata huduma za jamii
 • Kupata amri ya mahakama ya kupewa ulinzi
 • Kupata haki ya kulea watoto na matunzo ya watoto
 • Kutengana kisheria au kutalikiana bila idhini ya mwenzi wako

Kwa wahamiaji, ni muhimu pia kujua:

 • Unaweza kuripoti vitendo vya unyanyasaji bila kulazimika kushirikisha hali yako ya uhamiaji.
 • Una haki ya kupata msaada wa tafsiri ya lugha na ukalimani wakati unapoongea na polisi na unapopata huduma za serikali.
 • Una haki ya kupata msaada hata kama wewe ni mhamiaji asiye na vibali.

Pata msaada

Kuna huduma nyingi ambazo zinataka kukusaidia. Unaweza pia kupata msaada ambao ni maalum kwa watu kutoka nchi yako au wanaozungumza lugha yako.

Unaweza kuchukua hatua hizi za kwanza:

 • Andaa mpango wa usalama kujiandaa na tatizo. Hii inajumuisha kabla na baada ya kuondoka katika suala la unyanyasaji.
 • Weka kumbukumbu ya unyanyasaji wako. Piga picha majeraha yako na chukua picha za skrini za jumbe za vitisho.
 • Zungumza na mtu unayemwamini. Anaweza kuwa rafiki, mwanafamilia, mwalimu, mshauri wa shule, jirani, au kiongozi wa jumuiya.
 • Piga simu au tuma ujumbe mfupi kwenda simu ya usaidizi kwa msaada wa bure na bila kutoa utambulisho wako Simu za usaidizi zinajibiwa na wataalamu wenye mafunzo wanaoweza kutoa mwongozo na usaidizi.
 • Tembelea shirika la kijumuiya kwa msaada. Wanaweza kukupa usaidizi mbalimbali, ikiwemo ushauri nasaha, hifadhi, na ufikio wa rasilimali za kisheria.
 • Zungumza na wakili wa masuala ya uhamiaji. Pata ushauri kuhusu haki zako na chaguzi za ulinzi wa kisheria.
 • Tafuta msaada wa ustawi wako wa kiakili. Unyanyasaji unaweza kuathiri furaha na afya yako. Jifunze jinsi ya kupata huduma za afya ya akili.
Ukiwa na wasiwasi kwamba kuna mtu anafuatilia matumizi yako ya intaneti, futa historia ya kivinjari chako na tumia modi faragha (private mode). Unaweza pia kutumia kifaa cha rafiki yako au kompyuta ya maktaba kwa usalama zaidi.

Kuripoti ukatili wa majumbani

Ukatili wa majumbani ni kinyume cha sheria. Unaweza kuwaambia polisi kuhusu vitendo vya unyanyasaji wakati wowote.

Unaweza kufanya hivi:

 • Nenda kituo cha polisi au hospitali ikiwa unahitaji msaada wa matibabu. Unaweza kuripoti kwa polisi ukiwa hapo.
 • Ikiwa kuna dharura, zungumza na afisa wa polisi aliyekuja kusaidia. Kuwa mtulivu na sema ukweli.
 • Mjulishe polisi ikiwa mpenzi wako ana bunduki, silaha nyingine, hati ya kukamatwa, au amri ya zuio dhidi yake.
 • Ikiwa polisi watakuja nyumbani kwako, unaweza kuomba kuzungumza nao. Hulazimiki kusaini karatasi ambazo huwezi kuzisoma au huzielewi.
 • Angalia kama kituo au hifadhi mahalia wakati wa matatizo wanaweza kukusaidia kutoa ripoti.
 • Soma dondoo zaidi kuhusu kuripoti polisi.

Unaweza pia kuiomba mahakamani amri ya kupewa ulinzi inayomzuia mnyanyasaji kusogea karibu nawe au kukunyanyasa wewe na wengine. Utalazimika kutoa ushahidi katika kikao cha usikilizaji wa shauri. Amri ya kupewa ulinzi inaweza kudumu kwa miaka kadhaa na inawezekana kuirefusha.

Kila jimbo lina sheria maalum kuhusiana na ukatili wa majumbani. Jifunze kuhusu amri za zuio, talaka, haki ya kulea watoto na matunzo ya watoto katika jimbo lako.

Simu za usaidizi na msaada mwingine

Simu za usaidizi na mashirika hutoa usaidizi wa faragha na wa bure kwa manusura wa ukatili wa majumbani. Wanaweza kukusaidia na mpango wa usalama, kupata mahali salama pa kwenda, na kukupa usaidizi wa afya ya akili na ushauri wa kisheria.

Watakuomba taarifa kuhusiana na suala lako ili kujua chaguzi zipi zinapatikana kwako. Hulazimiki kuwashirikisha maelezo yoyote ambayo hutaki kuyatoa. Hawatashirikisha taarifa zako au kuripoti suala lako la kunyanyaswa bila ruhusa yako.

Shirika
Huduma
National Domestic Violence Hotline
800-799-7233
TTY 800-787-3224
Tuma ujumbe mfupi wa START kwenda 88788
Simu ya saa 24 inapatikana katika lugha 200+. Wanatoa pia huduma mahalia
Simu ya saa 24 kwa ukatili wa kingono. Inapatikana pia kwa Kispaniola.
Simu ya usaidizi kwa wahanga wa uhalifu.
Love is Respect
866-331-9474
TTY 800-787-3224
Simu ya saa 24 kwa watoto waliopevuka na vijana. Inapatikana pia kwa Kispaniola.
Womankind
888-888-7702
Simu ya saa 24. Inapatikana pia kwa Kispaniola na lugha 18 za Asia.
Simu ya saa 24 ya kupata mwongozo kuhusu unyanyasaji wa watoto. Hii si simu ya kuripoti vitendo vya unyanyasaji.
Taarifa za kisheria na usaidizi kupitia barua pepe.
Msaada wa kisheria kwa manusura wahamiaji.
Tafuta hifadhi na programu za ukatili wa majumbani karibu nawe.
Tafuta orodha ya mashirika yanayowasaidia manusura wa ukatili wa kingono.
Tafuta kituo karibu nawe.
Tafuta orodha ya mashirika ambayo yanaisaidia jumuiya ya Waislamu.
Rasilimali kuhusiana na unyanyasaji wa wazee.
Afghan Asylum Helpline
888-991-0852
Simu ya usadizi inayoweza kutoa msaada kwa lugha ya Dari na Pashto. 

Taarifa kwenye ukurasa huu umetoka kwa National Domestic Violence Hotline, USCIS, Esperanza United, na vyanzo vingine vinavyoaminika. Malengo yetu ni kutoa taarifa zilizo rahisi kuelewa na zinazosasishwa mara kwa mara. Taarifa hii si ushauri wa kisheria.

Share