Gawanya

Nini cha kufanya ikiwa mtu anakupa vitisho

Inaweza kuogopesha na kuumiza kichwa pale mtu anapokupa vitisho Ni muhimu kujua jinsi ya kukabiliana na vitisho na kujilinda. Fahamu hatua unazoweza kuchukua, jinsi ya kuripoti vitisho na kupata msaada.


Aina za vitisho

Kitisho ni pale mtu anaposema au kuonesha anataka kukudhuru wewe au mali yako. Hii inaweza kujumuisha kukudhuru kimwili au kihisia, kuharibu mali yako, matusi, kujaribu kukuogopesha, au kukunyanyasa. Kuna aina tofauti za vitisho na njia za kukabiliana navyo.

Kitisho cha ana kwa ana hutokea pale mtu wa karibu nawe anaonesha kutaka kukudhuru.

Kitisho cha simu hufanywa kupitia simu. Wakati mwingine vitisho vinavyotolewa kupitia simu vinaweza kuwa “simu za mzaha”. Hii ni pale mtu anapokufanyia utani na si kitisho cha kweli. Mara nyingi ni bora kuichukulia kama kweli ikiwa huna uhakika.

Kitisho cha ujumbe wa kielektroniki kawaida hupokelewa kupitia ujumbe wa maandishi, mitandao ya kijamii au barua pepe. 

Uhalifu wa chuki ni vitisho vinavyohusiana na rangi, dini, mwelekeo wa kingono, asili ya utaifa, au utambulisho mwingine. Kumekuwa na ongezeko la uhalifu wa chuki kwa Wamarekani wenye asili ya Asia wakati wa janga la COVID-19.

Jinsi ya kukabiliana na vitisho

Unachopaswa kufanya kinategemea na aina ya kitisho na ukubwa wa kitisho.

Ikiwa unatishiwa ana kwa ana:

  • Usalama wako ni muhimu zaidi. Angaza pande zote kwa haraka na utafute mahali salama pa kwenda. Hii inaweza kuwa mahali penye shughuli nyingi na watu wengi au mahali unapoweza kujificha.
  • Tulia. Epuka kutazamana machoni au kuongea na mtu anayekupa vitisho. Dumisha hali ya kawaida ya kimwili na ukimbie au urudi nyuma haraka.
  • Piga 911 kwa msaada wa haraka.
  • Omba msaada kutoka kwa watu walio karibu nawe.
  • Jifiche na jaribu kuziba njia ya kuja kwako. Nyamazisha simu yako.
  • Jaribu kukumbuka mambo muhimu kuhusu tukio hilo. Piga picha au video kama ni salama kufanya hivyo au muombe mtu wa karibu afanye hivyo. Ikiwa humfahamu mtu anayekutishia, angalia vitu vya kusaidia kumtambua mtu huyo kama vile umri wake, jinsia, rangi, urefu, uzito, nywele na rangi ya macho, mavazi, na kitu kingine chochote kilicho cha kipekee.
  • Pambana kama tu njia ya mwisho ikiwa maisha yako yapo katika hatari kubwa.
  • Ripoti kitisho kwa vyombo vya sheria.
Piga 911 ikiwa wewe au mtu mwingine yupo katika hatari kubwa. Fahamu nini cha kutarajia unapopiga simu polisi.

Ikiwa unapewa vitisho kwa njia ya simu au kwa ujumbe mfupi:

  • Tulia na usikate simu. Jaribu kupata taarifa zaidi kuhusu mtu anayekupa vitisho. Uliza maswali ili kusaidia kujua kama kitisho ni cha kweli.
  • Usijibu jumbe za simu, machapisho ya mitandao ya kijamii au barua pepe.
  • Tunza taarifa. Tunza jumbe za simu na kumbuka nambari ya simu au barua pepe. Piga picha ya vitisho vya mitandao ya kijamii. Ikiwezekana rekodi simu au kumbuka kile haswa kilichosemwa.
  • Ripoti kitisho kwa vyombo vya sheria.

Ikiwa kitisho kinahusiana na kuwa mhamiaji:

  • Tumia Kiingereza kama inawezekana.
  • Usihisi haja ya kuwaelimisha watu kuhusu imani zao potofu. Watu ambao ni wabaguzi wa rangi au wakatili hawana akili nzuri.
  • Tafuta msaada wa kisheria ikiwa mtu atatishia kuwapigia simu mamlaka za uhamiaji na unaogopa kufukuzwa nchini.
  • Ripoti uhalifu wa chuki kwa FBI.
  • Wasiliana na mashirika ya haki za kiraia, haswa ikiwa hutaki kuzungumza na vyombo vya sheria.
  • Fahamu haki zako kama mhamiaji.
  • Zungumza na watu wa jumuiya yako. Kuzungumza kuhusu vitisho na wengine ambao wamepitia mambo kama yako inaweza kukusaidia kujua la kufanya.
Baada ya kupewa kitisho, jaribu kutafuta usaidizi wa kihisia. Zungumza na mwanafamilia unayemwamini, rafiki, kikundi cha jamii, au tabibu wa afya ya akili. Fahamu zaidi kuhusu huduma za afya ya akili.

Ukishuhudia mtu fulani amekuwa mhanga wa kitisho:

  • Paza sauti au rekodi kitisho ikiwa ni salama kufanya hivyo.
  • Piga 911 ikiwa mhanga wa kitisho yupo katika hatari kubwa.
  • Zungumza na mhanga. Toa usaidizi na uliza jinsi unavyoweza kusaidia. Sikiliza matakwa yake kabla hujachukua hatua yoyote.
  • Jitolee kuondoka na mhanga.
  • Usimwache mhanga baada ya kitisho ikiwa anahitaji usaidizi zaidi.

Ripoti kitisho

Unaweza kuripoti vitisho vya kudhuru kwa vyombo vya sheria vya eneo lako au mashirika mengine yanayotoa msaada. Unaweza pia kuripoti vitisho kwa mamlaka fulani kulingana na eneo la kitisho husika.

Wasiliana
Kwa
911 wakati wa kitishoPolisi wa eneo hilo baada ya kitisho
Kitisho kikubwa mahali popote
Vitisho kwa haki zako za kiraia, ikiwemo haki za wahamiaji na LGBTQ+
Vitisho kwa haki za kiraia za Wamarekani wenye asili ya Afrika na uhalifu wa chuki
Vitisho kwa Wamerekani wenye asili ya Asia
Vitisho kwa haki za kiraia za Waislamu na uhalifu wa chuki
Vitisho kwa jumuiya za LGBTQ+
Vitisho nyumbani kwako
Ofisi mahalia ya FBI (800) 225‐5324
Vitisho vya mawakala wa serikali ya kigeni, maafisa wa serikali, njama za uhalifu, na uhalifu wa chuki
Meneja
Vitisho kwenye biashara, duka au mkahawa
Transit security
Vitisho katika usafiri wa umma
Mwalimu, mshauri, au mkuu wa shuleFahamu zaidi kuhusu usalama shuleni
Vitisho shuleni
Vitisho kwenye mitandao ya kijamii
Msimamizi wako auidara ya rasilimali watu
Vitisho mahali pako pa kazi

Ikiwa hutaki kuwapigia simu polisi, kuna rasilimali nyingine za usalama zinazopatikana kwako.

Unaweza kuripoti vitisho bila kujulikana. Mashirika ikiwemo polisi watashirikiana nawe kulinda utambulisho na usiri wako. Hawatashirikisha maelezo yako bila ya idhini yako.

Je, nini kitatokea baada ya kuripoti kitisho?

Kila shirika lina taratibu tofauti za kuchunguza na kushughulikia vitisho. Wasiliana na shirika lako kuhusu hatua zinazofuata.

Kwa kawaida, polisi watachunguza kitisho husika na mtu aliyetoa kitisho hicho. Ikiwa ulipiga picha au video, zinaweza kutumika kama ushahidi. Ikiwa polisi wataona kitisho hicho ni sadikifu na ni ukiukwaji wa sheria, wanaweza kutia mbaroni na kufungua mashtaka ya jinai. Kutishia kudhuru kimwili ni uhalifu mkubwa katika majimbo mengi.

Unaweza pia kufungua kesi ya madai katika mahakama kwa madhara ya kihisia au kimwili. Unaweza kufungua kesi ya kupewa amri ya zuio dhidi ya mtu ili aache kukupa vitisho na akae mbali nawe.

FindHello app Houston search map
Find help near you

Find legal help, English classes, health clinics, housing support, and more. Search a local map and list of services for immigrants in the USA with the app FindHello.

Start your search

Taarifa kwenye ukurasa huu umetoka kwa USA.gov, the FCC, na vyanzo vingine vinavyoaminika. Malengo yetu ni kutoa taarifa zilizo rahisi kuelewa na zinazosasishwa mara kwa mara. Taarifa hii si ushauri wa kisheria.

Share