Jinsi ya kupata wakili wa uhamiaji bila malipo na msaada wa kisheria wa gharama nafuu

Umerekebishwa Januari 24, 2024
Ukurasa huu ulitafsiriwa kitaalamu na mwanadamu. Jifunze zaidi

Ni muhimu kupata ushauri wa kisheria wakati wa kuomba mafao ya uhamiaji au ikiwa upo kizuizini. Mashirika mengi hutoa msaada wa kisheria wa bure au wa gharama nafuu na wakili wa uhamiaji au mwakilishi aliyeidhinishwa. Jifunze jinsi ya kupata msaada wa kuaminika na jinsi unavyoweza kujiwakilisha.

Msaada wa kisheria ni nini?

Msaada wa kisheria ni ushauri kuhusu sheria na uwakilishi mahakamani. Wanasheria, mawakili, na wawakilishi walioidhinishwa wanaweza kutoa msaada wa kisheria. Nchini Marekani, maneno mwanasheria na wakili mara nyingi hutumiwa kwa njia ileile.

Wanasheria wataalam katika maeneo tofauti kama vile jeraha la mtu binafsi, sheria ya jinai, mali isiyohamishika, na masuala ya familia. Ukurasa huu unaangazia msaada wa uhamiaji lakini pia unatoa nyenzo chache kwa mahitaji mengine ya kisheria.

Pro bono ni kazi inayofanywa na wakili bila malipo. Ni msaada wa kisheria unaotolewa kwa watu wenye kipato cha chini.

Kwa nini ni muhimu kupata msaada wa kisheria?

Huna haja ya kuwa na mwanasheria lakini mchakato wa uhamiaji nchini Marekani ni ngumu. Wakili wa uhamiaji anaweza kukusaidia kuwasilisha fomu za uhamiaji na kukutetea mahakamani. Una nafasi nzuri zaidi ya kupata msaada wa kisheria.

Mwanasheria wa uhamiaji anaweza kufanya kazi ili kupata faida za uhamiaji kama vile Green Card, hifadhi, au uraia. Wanaweza kukusaidia:

  • Kuchunguza machaguo yako na hatua zinazofuata
  • Kuelewa maswali kuhusu maombi na fomu zako
  • Kuepuka makosa kwenye maombi yako ambayo yanaweza kusababisha kesi yako kukataliwa
  • Wasilisha ombi lako na hati za ushahidi
  • Jitayarishe kwa mahojiano yoyote na utafute mkalimani
  • Pata taarifa na maamuzi ya kesi yako
  • Boresha nafasi zako za kushinda kesi yako
  • Kukata rufaa ya uamuzi

Je, ni wakati gani ninapaswa kupata msaada wa kisheria?

Unaweza kupata msaada wa kisheria wakati wowote. Ikiwa unatafuta msaada kubadilisha hadhi yako ya uhamiaji, ni bora kupata mtu ambaye atapitia maombi yako kabla ya kuyatuma. Mara zote wanasheria wa uhamiaji hawapo wa kutosha kwa kila kesi. Wakati mwingine inaweza kuchukua muda mrefu kupata msaada sahihi.

Ni muhimu kupata msaada wa kisheria ikiwa uko katika kesi za kuondolewa katika mahaka ya uhamiaji. Serikali haitoi ushauri wa bila malipo kwa watu walio katika kesi za uhamiaji. Utapatiwa orodha ya huduma za kisheria za bila malipo au za gharama nafuu ambazo unaweza kuwasiliana nazo.

Ukiachilia mbali uhamiaji, kuna wakati mwingine ambapo kuwa na mwanasheria ni jambo muhimu. Hii inaweza kujumuisha masuala ya sheria ya familia, maswala ya ajira au nyumba, kesi za jinai, kuelewa hati za kisheria na mikataba, shida za kupata faida za umma, madai ya majeraha ya mtu binafsi, na kuanzisha biashara.

Nani anaweza kunipa msaada wa kisheria?

Wataalamu wafuatayo wanaweza kutoa ushauri wa kisheria na huduma katika kesi za uhamiaji na uraia:

  • Mwanasheria wa Uhamiaji au wakili: aliyepewa leseni na chama cha wanasheria wa jimbo kutoa msaada wa kisheria. Wakili amehitimu shule ya sheria na ana shahada ya Udaktari wa Sheria (J.D.).
  • Mwakilishi aliyeidhinishwa na DOJ: shirika la mtu binafsi au lisilo la faida alifundishwa kutoa huduma za uhamiaji na limeidhinishwa na Department of Justice (DOJ).

Wakili wa uhamiaji na mwakilishi aliyeidhinishwa kikamilifu wanaweza kukuwakilisha mbele ya DHS, USCIS, EOIR (mahakama ya uhamiaji), na BIA (rufaa ya uhamiaji). Mwakilishi aliyeidhinishwa kiasi anaweza kukuwakilisha tu mbele ya USCIS.

Ninawezaje kupata msaada wa kisheria ambao ninaweza kuamini?

Ikiwa unatafuta msaada na kesi ya uhamiaji, hakikisha unazungumza na wakili ambaye ana uzoefu katika sheria ya uhamiaji. Wakili ambaye hana utaalam katika sheria ya uhamiaji hawezi kukupa ushauri sahihi.

Pia, fahamu kwamba shughuli zingine zinajifanya kutoa huduma za kisheria za kuaminika ili kupata pesa. Kuna baadhi ya mambo rahisi unaweza kufanya ili kujilinda.

Kwa wakili wa uhamiaji:

Kwa mwakilishi aliyeidhinishwa:

  • Muombe akuonyeshe uthibitisho wa kibali
  • Angalia kama yupo kwenye orodha ya DOJ

Vidokezo vya ziada:

  • Machaguo ya utafiti na wasiliana na mwanasheria zaidi ya mmoja
  • Muulize kama anatoa ushauri wa bure
  • Uliza maswali kuhusu aina ya kesi wanazoshughulikia na huduma wanazotoa
  • Uliza kuhusu utaratibu mzima wa ada na malipo yanayohitajika kabla ya kuanza
  • Tenga muda wa kukagua mkataba au makubaliano yoyote kabla ya kusaini
  • Uliza kama wana kiwango cha ada kulingana na uwezo wa mtu ili kukusaidia kulipa gharama
Kiwango cha ada kulingana na kipato inamaanisha gharama ya huduma ya wakili inategemea mapato yako. Kadiri unavyopata pesa kidogo katika kazi yako, ndivyo unavyolipwa kidogo kwa usaidizi wa kisheria.

Epuka udanganyifu na uwe mwangalifu na mtu yeyote ambaye:

  • Husalimiana na wewe kwanza
  • Inatoa mabo ambayo yanaonekana kuwa ni ya kweli
  • Hutoa dhamana au ahadi za faida
  • Hutoa huduma za kisheria kwa kubadilishana na kitu
  • Anakataa kuweka mkataba au makubaliano
  • Hujaribu kuhifadhi hati zako halisi
  • Gharama za fomu tupu za uhamiaji
mwanasheria anayekagua taarifa
Epuka ulaghai wa uhamiaji

Fahamu jinsi ya kujilinda mwenyewe dhidi ya wathibitisha na tovuti bandia. Jifunze nini cha kufanya unapokuwa mwathirika wa udanganyifu.

Pata Maelezo Zaidi

Ninaweza kupata wapi msaada wa kisheria wa bila malipo au wa gharama nafuu?

Unaweza kupata mawakili wa uhamiaji na wawakilishi walioidhinishwa na DOJ ambao hutoa msaada wa bila malipo au wa gharama nafuu kupitia mashirika yasiyo ya faida. Pia, unaweza kuwauliza watu unaowaamini wakupe mapendekezo.

Rasilimali
Msaada
Orodha ya wanasheria wa uhamiaji. Kila mmoja anaweza kulipisha ada tofauti kulingana na kesi yako. Wasiliana nao moja kwa moja ili kujua kama wanatoa ushauri bila malipo
Kuwa mwanachama wa ASAP hukupa fursa ya kupata mawakili waliobobea wa uhamiaji, watafuta hifadhi wengine, na nyenzo muhimu bila malipo
Jiunge na msaada wa kisheria wa bila malipo, mubashara, wa mtandaoni ili ukusaidie katika mchakato wako wa uraia
Kitabu cha mtandaoni cha orodha ya mashirika yasiyo ya faida yanayotoa huduma za kisheria za uhamiaji za bila malipo au za gharama nafuu. Tafuta msaada wa kisheria kwa jimbo, msimbo wa posta, kizuizi, eneo la uhamiaji, na aina za huduma
Inatoa nyenzo za kisheria kwa jamii za wahamiaji wa LGBTQ+na/au wenye HIV, pamoja na taarifa kuhusu hifadhi na kizuizi
Namba ya simu kwa wakimbizi na wanaotafuta hifadhi ili kuzungumza na mtu kwa ajili ya msaada. Piga simu 202-461-2356 au #566 kutoka kwenye simu ya kizuizini
Tafuta mashirika na vituo vya msaada kama wewe au mpendwa wako amezuiliwa au ametenganishwa na familia

Kama unatafuta msaada wa kisheria nje ya Marekani, pata taarifa kwenye ukurasa wetu msaada wa kimataifa.

Ramani ya utafutaji wa Houston wa programu ya FindHello
Kupata msaada ulio karibu na wewe

Pata msaada wa kisheria, madarasa ya Kiingereza, kliniki za afya, msaada wa nyumba, na zaidi. Tafuta ramani ya eneo lako na orodha ya huduma kwa wahamiaji nchini Marekani na programu ya FindHello.

Anza utafutaji wako

Ninawezaje kupata msaada ikiwa ninajiwakilisha?

Ikiwa unajikilisha katika mahakama ya uhamiaji, kuna nyenzo za kukusaidia.

Pro se ni neno linalotumika pale ambapo mtu fulani anajiwakilisha mahakamani na hana mshauri wa kisheria. Ni Kilatini likimaanisha "kwa niaba ya mtu mwenyewe."

Kuna msaada wa kisheria unaopatikana katika maeneo ya nje ya uhamiaji. Ofisi nyingi za misaada ya kisheria hutoa msaada wa bila malipo au wa gharama nafuu kwa watu ambao wana matatizo katika maswala ya watumiaji, unyanyasaji wa familia na majumbani, nyumba, faida za umma, na ajira.

  • American Bar Association hutoa nyenzo za kupata msaada wa kisheria wa bila malipo.
  • LawHelp.org ina miongozo ya taarifa za kisheria na orodha ya mipango ya bila malipo ya msaada wa kisheria.
  • Law Help Interactive ina miongozo ya bila malipo ya jinsi ya kujaza fomu za kisheria.

Haki zangu ni zipi?

Kila mtu ana haki ya kupata msaada wa kisheria. Hawatateua wakili bure kwa ajili yako katika mahakama ya uhamiaji. Ni wajibu wako kutafuta msaada wa kisheria. Utapewa orodha ya watoa huduma wa kisheria wa bila malipo au wa gharama nafuu katika mahakama ya uhamiaji.

Unaweza kuwasilisha malalamiko dhidi ya wakili wako kwenye chama chao cha jimbo au kwenye Executive Office for Immigration Review. Unaweza kubadilisha wanasheria ikiwa wakili wako haelezei machaguo yako katika kesi za uhamiaji au hajawasilisha nyaraka zinazohitajika. Wewe au wakili wako mpya anaweza kuomba nakala ya faili ya kesi yako.

Unapaswa kuripoti utapeli wa uhamiaji kwa USCIS, Executive Office for Immigration Review, au Tume ya Taifa ya Biashara.


Taarifa kwenye ukurasa huu inatoka LawHelp.org, the National Immigrant Justice Center, the Department of Justice, UNHCR, na vyanzo vingine vinavyoaminika. Tunakusudia kutoa taarifa rahisi kueleweka ambazo zinarekebishwa mara kwa mara. Taarifa hii sio ushauri wa kisheria.