Marufuku mpya ya kusafiri
Mnamo Juni 4, 2025, utawala wa Trump ulitangaza marufuku mpya ya kusafiri inayozuia au kuweka vikomo vya kuingia Marekani kwa watu kutoka baadhi ya nchi.
Mnamo Desemba 16, 2025, nchi zaidi ziliongezwa kwenye orodha hii au sasa zitakuwa chini ya vizuizi vikali zaidi. Hizi zimewekwa alama ya nyota (*). Vikwazo hivi vitaanza kutumika mnamo Januari 1, 2026.
Kuna aina mbili za vikwazo: marufuku kamili ya kusafiri na marufuku ya kusafiri kwa sehemu fulani.
1. Marufuku kamili ya kusafiri kwa nchi 20
Watu kutoka nchi na maeneo haya hawaruhusiwi kuingia Marekani isipokuwa ikiwa wanakidhi vigezo vya hali maalum:
- Afghanistan
- Burkina Faso*
- Burma
- Chad
- Jamhuri ya Kongo
- Guinea ya Ikweta
- Eritrea
- Haiti
- Iran
- Laos*
- Libya
- Mali*
- Niger*
- Wamiliki wa hati za kusafiri zilizotolewa na Mamlaka ya Palestina*
- Sierra Leone*
- Somalia
- Sudan Kusini*
- Sudan
- Syria*
- Yemen
Hali maalum (kumaanisha kuwa unaweza bado kuingia) ni pamoja na:
- Ikiwa unatoka kwenye nchi iliyo kwenye orodha marufuku ya kusafiri ya Juni 2025 (bila nyota *) na una visa halali kufikia Juni 9, 2025
- Ikiwa unatoka kwenye nchi iliyo kwenye orodha ya marufuku ya kusafiri ya Januari 2026 (yenye nyota *) na una visa halali kufikia Januari 1, 2025
- Watu wenye Green Card (Wakazi halali wa kudumu)
- Raia wenye uraia wa nchi mbili wanaosafiri kwa kutumia pasipoti ya nchi ambayo haiko kwenye orodha
- Wamiliki fulani wa visa za kidiplomasia na rasmi (A, G, NATO)
- Baadhi ya makundi ya kidini au kikabila madogo kutoka Iran
- Wanariadha na wafanyakazi wao wanaohudhuria matukio makubwa ya kimataifa
Wamiliki wa SIV wa Afghan , baadhi ya SIV zinazohusishwa na serikali ya Marekani na ndugu wa karibu wa raia wa Marekani watajumuishwa katika marufuku iliyopanuliwa ya usafiri itakayotolewa Januari 1. Makundi haya hayatakuwa na idhini maalum tena. Ni katika hali nadra sana ambapo serikali ya Marekani itazingatia hali maalum.
Muhimu:
- Ikiwa unatoka katika mojawapo ya nchi zilizopigwa marufuku kusafiri na uondoke nchini Marekani, huenda usiruhusiwe kurudi. Hata kama una idhini maalum (kwa mfano, una Green Card), unaweza kukumbana na matatizo unapojaribu kuingia tena nchini Marekani.
- Ukisafiri kwenda mojawapo ya nchi hizi (hata kama hutoki katika nchi hiyo), unaweza kukumbana na uchunguzi wa ziada au matatizo ya kuingia tena, hasa kama wewe si raia wa Marekani.
- Aina za visa zilizojumuishwa kwenye marufuku (kumaanisha kuwa haziwezi kutumika kuingia) ni pamoja na:
- Visa za F2A na F2B (wenzi wa ndoa na watoto wa wamiliki wa Green Card)
- Washindi wa visa anuai (DV)
- Visa za msingi wa ajira (H, L, O, n.k.)
- Viza za wanafunzi na wageni (F, M, J, B)
- Visa za mchumba za K-1
- Kesi za kufuata kujiunga (I-730) kwa waomba hifadhi na wakimbizi zinaweza kuendelea. Kesi nyingi za wanaofuata kujiunga za mhifadhiwa zinachakatwa nje ya nchi na wataruhusiwa kusafiri, lakini wanufaika sharti wagharamie wenyewe uchunguzi wa kitabibu na gharama za kusafiri. Hata hivyo, kesi za fuata kujiunga za mhifadhiwa kutoka nchi zilizotajwa katika nchi zenye marufuku ya kusafiri zinakataliwa baada ya mahojiano ya kibalozi. Kesi nyingi za wakimbizi za fuata kujiunga bado zimesitishwa nje ya nchi. Kusafiri kwenda Marekani pia kumesitishwa.
2. Vikwazo kwa sehemu fulani kwa nchi 20
Baadhi ya wasafiri kutoka nchi hizi bado wanaweza kuingia Marekani, lakini aina fulani za visa zimewekewa vikwazo:
- Angola*
- Antigua na Barbuda*
- Benin*
- Burundi
- Cote d’Ivoire*
- Cuba
- Dominika*
- Gabon*
- Gambia*
- Malawi*
- Mauritania*
- Nigeria*
- Senegal*
- Tanzania*
- Togo
- Tonga*
- Turkmenistan
- Venezuela
- Zambia*
- Zimbabwe*
Marufuku ya Turkmenistan sasa inawazuia raia wa Turkmen kuingia kwa kutumia visa za wahamiaji. Marufuku ya visa za wageni wa Turkmen itaondolewa. Laos na Sierra Leone zilikuwa na vikwazo kwa sehemu fulani, lakini kuanzia Januari 1, 2026, zitakuwa na chini vizuizi kamili.
Vikwazo vya sehemu inamaanisha:
- Hakuna visa mpya za wahamiaji (za kuingia Marekani kama mkazi halali wa kudumu)
- Hakuna visa zisizo za wahamiaji katika kategoria za B, J, F, au M
- Muda mfupi wa ustahiki wa visa kwa kategoria zingine zisizo za wahamiaji
- Muda mrefu zaidi wa uchunguzi na uchakataji
- Hati za ziada au mahojiano
- Maswali zaidi kwenye uwanja wa ndege au mpakani
- Wamiliki wa Green Card kutoka nchi hizi hawapaswi kuathirika
Hata kama marufuku ya kusafiri haitumiki kwako, safari za kimataifa bado zinaweza kuwa hatari ikiwa wewe si raia wa Marekani. Kusafiri kwa ndege ndani ya Marekani pia kunaweza kusababisha hatari za utekelezaji wa sheria za uhamiaji. Unaweza kuhitaji hati ya kusafiri. Pata Maelezo Zaidi.
Sheria zaidi kwa watu kutoka nchi zilizopigwa marufuku ya kusafiri
Ikiwa unatoka katika mojawapo ya nchi zilizoorodheshwa hapo juu:
- Maombi ya uhamiaji yamezuiliwa kwa muda. Ikiwa tayari umeomba mafao, ikijumuisha Green Card na uraia, kesi yako imesitishwa.
Ikiwa unatoka katika nchi iliyoorodheshwa kwenye marufuku ya usafiri ya Juni 2025:
- Mafao ya uhamiaji yanakaguliwa tena kwa watu walioingia Marekani mnamo au baada ya tarehe 20 Januari 2021. Ikiwa uliidhinishwa kupata mafao, kama vile Green Card, kesi yako inaweza kukaguliwa tena.
- Wamiliki wa Green Card wanaweza kukaguliwa tena. Ikiwa una Green Card, unaweza kufanyiwa ukaguzi au mahojiano tena. Taratibu hizi za mahojiano ya pili bado hazijaanza.
- Unaweza kukumbana na ukaguzi zaidi wa usalama. USCIS sasa itachukulia wasiwasi wa usalama na matatizo ya kuthibitisha hati za utambulisho kama mambo hasi wakati wa kukagua kesi fulani za uhamiaji.
USCIS inakagua upya kesi za wakimbizi kuanzia Januari 20, 2021 hadi Februari 20, 2025. Ikiwa uliingia nchini kupitia mpango wa mkimbizi kwa wakati huu, hakuna mabadiliko ya haraka kwa hali yako ya sasa, lakini kesi yako inaweza kuchunguzwa tena. Maombi ya Green Card yanayosubiri ya kikundi hiki pia yamesitishwa.
Zaidi kutoka USAHello
Je, unatafuta taarifa mahususi?
Taarifa kwenye ukurasa huu inatoka USCIS na vyanzo vingine vinavyoaminika. Tunakusudia kutoa taarifa rahisi kueleweka ambazo zinarekebishwa mara kwa mara. Taarifa hii sio ushauri wa kisheria.