Kaa salama ukiwa na taarifa za kweli

Ukurasa huu ulisasishwa mwisho 5/25/2020. Kwa sasisho baada ya hiyo tarehe, tafadhali nenda kwa ukurasa wa Kiingereza

Kuna habari nyingi kuhusu virusi vya corona. Je, unafahamu zipi ni za kweli na zipi sizo? USAHello ina taarifa kutoka vyanzo tunavyoweza kuviamini. Tazama video zetu kuhusu uongo juu ya virusi vya korona. Jifunze juu ya utapeli kuhusu virusi vya korona ili uwe salama.

Nini ni kweli na uongo kuhusu virusi vya korona?

Tazama video za wafanyakazi, wanaojitolea na wajumbe wa bodi wa USAHello ili kuelewa kipi ni kweli na kipi ni uongo kuhusu taarifa za virusi vya korona.

Video za USAHello zinapatikana kwa lugha nyingi!

Chukua tahadhari dhidi ya utapeli wa virusi vya korona

Utapeli ni ulaghai. Kawaida, watu wanaowatapeli watu wengine hujaribu kuwadanganya na kuwaibia hela zao. Wakati mwingine tunapokuwa na hofu ni vigumu kutofautisha kilicho kweli na kisicho. Hizi ni baadhi ya utapeli ambao sote inatubidi tuujue!

Namna ya kuepuka taarifa mbaya

Watu wengi hawamaanishi wanaposambaza taarifa mbaya. Lakini zipo taarifa nyingi potofu zitokazo kwa wanajamii. Sote tunaweza kueneza taarifa njema badala yake!

Taarifa hizi zimetokana na vyanzo vya kuaminika, kama vile UNICEF, the Kituo cha Kudhibiti Magonjwa na Shirika la Afya Dunian. USAHello halitoi ushauri wa kisheria au kimatibabu, wala rasilimali zetu hazikusudiwi kuchukuliwa kama ushauri wa kisheria au kimatibabu.

Je, una maswali zaidi kuhusu namna ya kupata taarifa za ukweli? Unaweza kuuliza [email protected].